Mgombea Ubunge Jimbo la Malinyi, kupitia NCCR-Mageuzi, Kennedy Chaya, amesema ikiwa wananchi watamchagua, atahakikisha inaanzishwa Hifadhi ya Wanyamapori ya Malinyi.

Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya kampeni, Chaya alisema katika wilaya ya Malinyi kuna mbuga kubwa na ndani yake kuna wanyama wa kila namna katika mbuga hiyo, ambayo kwa sasa serikali inaitambua kama pori tengefu.

Chaya alisema wilaya hiyo itakapokuwa na hifadhi kutakuwa na faida kubwa kwa kupata fedha za kigeni na kwamba mapato ya ndani yataongezeka na ajira zitakuwa nyingi kwa vijana.

Kuhusu elimu, alisema pamoja na serikali kutoa elimu bure kutoka shule za msingi hadi sekondari, ziko changamoto nyingi katika jimbo hilo ikiwamo uhaba wa walimu, vyumba vya madarasa na vifaa vya kufundishia hali ambayo inasababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu.
Mgeni rasmi wa kongamano la unyonyeshaji linalojulikana kama Mother Meer Up event lililoandaliwa na USAID TULONGE AFYA mjini Iringa Dkt Jescar Leba (mganga mkuu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa) akiongea na akinamama wakati wa kongamano hilo.
Mmoja wa akina mama waliohudhuria kongamano la onyonyeshaji linalojulikana kama Mother Meet Up event lililoandaliwa na USAID TULONGE AFYA mjini Iringa Pendo Muhongole akifuatilia kwa makini maelezo ya mgeni rasimi kwenye kongamano hilo

Mganga mkuu wa halmashauri ya manispaa ya Iringa Dokta Jescar Leba amewataka wakinamama wanaojifungua kufuata maelekezo ya wataalamu ikiwemo kutowaongezea chakula chochote watoto pindi wanapozaliwa hadi kufikia umri wa miezi sita kwa lengo la kulinda afya zao.

Dokta Leba ametoa rai hiyo kwenye shughuli ya wakina mama wenye watoto chini ya miezi 6 ijulikanayo kama “Mother Meetup” iliyoandaliwa na na mradi wa USAID TULONGE AFYA kupitia jukwaa la NAWEZA kwa lengo la kuwakumbusha wakinamama hao juu ya malezi bora ya watoto ambapo amesema watoto wanaozaliwa hawapaswi kuongezewa chakula chochote kwakuwa nyongeza hiyo ya chakula inaweza kuathiri afya na ukuaji wao kimwili na kiakili.

Aidha Dokta leba ameongeza kuwa zipo mila na desturi mbaya zilikuwa zinaathiri kampeni hiyo lakini kwa juhudi za serikali na wadau wa maendeleo, jamii imeelewa umuhimu wa unyonyeshaji maziwa ya mama pekee na kuanza kufuata utaratibu huo na kuongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu walizonazo kwasasa unyonyeshaji bila nyongeza ya chakula kwa miezi sita ni karibu asilimia mia moja

“Tulikuwa na changamoto ya mila na desturi katika eneo hili ambapo wazazi walikuwa wakishinikizwa na wanafamilia mfanobibi au majirani kwamba mtoto akilia anapaswa kupewa uji au hata maji kwa madai kuwa maziwa ya mama pekee hayatoshi lakini kwa sasa wengi wamekwishaelewa na utekelezaji ni karibu asilimia mia moja”. Aliongeza Dokta Leba

Baadhi ya wakinamama hao wametoa ushuhuda na kueleza kuwa changamoto ya mila na desturi ilikuwa kikwazo kutokana na jamii inayowazunguka kulazimisha watoto kupewa nyongeza ya chakula ndani ya muda mfupi wa kuzaliwa kwa madai kuwa maziwa yam am hayawezi kumtosheleza

“Mimi nilipojifungua ndani ya kipindi cha wiki mbili mtoto wangu wa kwanza alikuwa analia sana ndipo nikaambiwa nimuongezee chakula kwa madai kuwa maziwa yangu yalikuwa hayatoshi. Lakini nilikataa na kuendelea kumnyonyesha mwanagu mpaka alipofikisha miezi sita ndipo nikaanza kumuongezea vyakula na mpaka sasa ana afya njema”. alisema bi. Theresia Joseph ambaye ni mama wa watoto wawili

Sezaria Andrew ni yeye ni mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wa manispaa ya Iringa alisema pamoja na hamasa iliyofanywa na serikali katika kuhakikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa kipindi cha miezi sita unazingatiwa, mchango wa wadau wa maendeleo kupitia miradi mbalimbali kama mradi wa USAID Tulonge Afya si wakubezwa katika mafanikio yaliyofikiwa kwenye kampeni hiyo.

“Tunawashukuru wadau wetu USAID TULONGE AFYA kwani wamekuwa kiungo cha mabadiliko ya tabia ndani ya jamii, ,tunawaomba waendelee kutuunga mkono ili tuendelee kumpambania mtoto wa kitanzania. Watoto wanaoanzishiwa chakula kabla ya miezi sita ya kuzaliwa wengi husumbuliwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya tumbo kutokana na utumbo kutokuwa na uwezo wa kuchakata chakula” alisema dokta Sezarina Andrew.

Mradi wa USAID Tulonge Afya ni mradi miaka mitano unatekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na shirika la FHI360 na wadau wengine wakiwamo mashirika ya TCDC na TMARC chini ya ufadhili wa shirika la kimarekani lijulikanalo kama USAID. Mradi huu unatekelezwa hapa nchini katika Wilaya 29 kwenye mikoa 12. Kwa upande wa mkoa wa Iringa mradi unatekelezwa katika wilaya tattu ambazo ni Iringa Manispaa, Mufindi DC na Kilolo DC. 

Baadhi ya akinamama wakifuatilia mafunzo juu ya namna bora ya kunyonyesha sambamba na suala zima la malezi ya mtoto, mafunzo hayo yaliyofanyika mjini Musoma jana ambayo yakiitwa Mother Meet Up event huku yakiandaliwa na Shirika la FHI360 chini ya ufadhili wa Shirika la misaada la Marekani la USAID.
Mratibu wa Huduma za mama na mtoto Manispaa ya Musoma, Deborah Mkama akimuelekeza mama jinsi ya kumnyonyesha mtoto wakati wa mafunzo ya namna ya unyonyeshaji ya Mother Meet Up Event yaliyoandaliwa na Shirika la FHI360 chini ya ufadhili wa Shirika la misaada la Marekani la USAID mjini Musoma jana.

Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na Rorya mkoani Mara zanufaika na mradi wa USAID Tulonge Afya unaolenga kutoa elimu katika jamii ili kubadili tabia hasi ili kuweza kuisaidia jamiii kuwa na Afya njema..

Akizungumza mjini hapa jana kwenye shughuli ya wakina mama wenye watoto chini ya miezi sita ijulikanayo kama “Mother Meetup” iliyoandaliwa na na mradi wa USAID TULONGE AFYA kupitia jukwaa la NAWEZA kwa lengo la kuwakumbusha wakinamama hao juu ya malezi bora ya watoto Mratibu wa asasi ya OWSL, Dk. Theophil Kayombo dhumuni la kuwakutanisha kina mama hao ni kuwapa nafasi ya kuweza kupeana uzoefu na kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo malezi ya watoto kuanzia wanapozaliwa mpaka kufikia umri wa miaka mitano.

Aidha Dkt, Kayombo aliainisha mambo hayo kuwa ni Umuhimu wa kunyonyesha maziwa ya mama pekee yake kwa kipindi cha miezi sita ya mwanzo bila kumpatia mtoto vyakula vya ziada , baada ya kujifungua umuhimu wa kutumia njia za kisasa za Afya ya UZAZI ili kuzuia kupata mimba nyingine ndani ya miaka miwili. Ili kuruhusu mtoto kukua na kuwa na afya bora , kuhakikisha mama na Mtoto mchanga analala ndani ya chandarua kilichotiwa dawa ili kujikinga na ugonjwa wa Malaria, pamoja na umuhimu wa kumpeleka mtoto mchanga katika kituo cha kutolea huduma za afya mara tu unapogundua dalili za ugonjwa.


Ameongeza kuwa kupitia mradi wa Tulonge Afya wanawafikia jamiii kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na uundwaji wa vikundi,elimu kwa njia mbalimbali lengo likiwa ni kuwafikia walengwa katika makundi yao ili waweze kuelimika na kufuata kanuni bora za afya kama inavyoelekezwa na wataalam.

Mratibu wa uhamasishaji huduma za jamii kutoka ofisi ya mganga mkuu wa manispaa ya Musoma, Dk. Magreth Shaku aliishukuru asasi hiyo kwa kuamua kutekeleza mradi huo ndani ya manispaa ya Musoma kwa maelezo kuwa mradi huo umekuja muda muafaka hivyo utasaidia katika kuongeza uelewa wa jamii juu ya masula mbalimbali ya afya ikiwemo suala la kunyonyesha watoto hasa katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo mtoto anapozaliwa.

Dk. Shaku alisema kuwa suala la unyonyeshji wa watoto bado linakabaliwa na changamoto mbalimbali zinazopelekea akinamama kushindwa alkunyonyesha kama inavyoshauriwa kitaalam hali ambayo kwa namna moja ama nyingine imekuwa ikileta changamoto katika suala zima la makuzi ya mtoto.

Alizitaja baadhi ya changamoto kuwa ni pamoja na baadhi ya akinamama kukataa kunyonyesha watoto wao wakidai kuwa maziwa yao yataanguka pamoja na ushiriki hafifu wa akinababa kwenye suala zima la malezi ya mtoto.

Aliwataka akinamama kuhakikisha kuwa wananyonyesha watoto ipasavyo kwa maelezo kuwa mbali na unyonyeshaji kuwa na manufaa katika makuzi ya watoto lakini pia ni njia kuu mojawapo ya kumkinga mama dhidi ya ugonjwa wa saratani ya matiti.

Naye mratibu wa mradi huo, Cyprian Lungu, alisema Mradi wa USAID Tulonge Afya ni mradi miaka mitano unatekelezwa na serikali kwa kushirikiana na shirika la FHI360 na wadau wengine chini ya ufadhili wa shirika la kimarekani lijulikanalo kama USAID. Mradi huu unatekelezwa hapa nchini katika Wilaya 29 kwenye mikoa 12. Kwa upande wa mkoa wa Mara mradi unatekelezwa katika wilaya mbili ambazo Musoma Manispaa na Rorya 

Aliongeza kuwa mradi huo unalenga kuleta mabadiliko ya tabia kwa kupambana na tabia hasi katika jamii zinazouia wanajamii kupata huduma bora za afya.

Alisema kuwa akinamama watapata elimu juu ya namna wanavyotakiwa kujiandaa kiafya kabla na baada ya kujifungua pia namna bora ya kuwalea watoto wao katika umri wa chini ya miaka mitano jambo ambalo litasaidia kuwa na jamii iliyo bora.
Nahodha wa timu ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Ally Samata (katikati) akiwa ameshatia saini kandarasi ya miaka minne ya kukitumikia kikosi cha Fenerbahnce kilichopo nchini Uturuki kwa euro milioni 8 akitokea Aston villa inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza.

MSHAMBULIAJI nyota wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta rasmi amesaini kandarasi ya miaka minne na kujiunga na miamba ya jiji la Istanbul, Fenerbahce akitokea Aston villa kwa dau ya euro milioni 8.

Klabu ya Fenerbahce imethibitisha rasmi kuinasana saini ya mshambuliaji huyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii za Instagram na Twitter.

Klabu ya Aston villa, kupitia ukurasa wake wa Instagram imemtakia kila la heri nyota huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania katika maisha mapya ya soka akiwa Fenerbahce.

Samatta alijiunga na Aston villa Januari mwaka huu akitokea Genk ya ubeligiji kwa dau la Paundi milioni 10.

Samatta amekuwa hana wakati mzuri katika kikosi cha Aston villa chini ya kocha Dean Smith, na kupelekea kutopata nafasi katika kikosi cha kwanza, katika msimu mpya ulioanza Semptemba 12. 

Inaelezwa kuwa huenda ujio wa Ollie Watkins kutoka Brentford, ikawa sababu ya Samatta kuondoka villa park.
Mtafiti kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya kuandaa shamba, kulipima na upandaji wa zao la korosho kwa Maafisa Ugani na Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa katika shamba la Shule ya Sekondari ya Mnyakongo.
Mtafiti kutoka Tari- Naliendele Programu ya Zao la Korosho, Kasiga Ngiha, akitoa mafunzo ya jinsi ya upimaji wa shamba kabla ya kupanda korosho.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Songambele, Asha Malekela wa Wilaya ya Kongwa akipima shamba kwa kamba katika mafunzo hayo kwa vitendo.
Maafisa Ugani na Wakulima wakijifunza kwa vitendo namna ya upimaji wa shamba la korosho kabla ya kupanda.
Mkulima Gasper Rupia kutoka Kijiji cha Ibwaga, akijifunza namna ya kupima shamba wakati wa mafunzo kwa vitendo. Kulia ni Mkulima Raheli Esau kutoka kijiji hicho.
Afisa Kilimo, Said Kajagale kutoka Kata ya Ngomai akijifunza kunyoosha mstari kwa kuelekeza kwa mkono katika mafunzo hayo ya vitendo.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Mkoka, Marcelin Chingilile (kushoto) na wenzake wakiwa kwenye mafunzo hayo
Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Kongwa, Elias Chilemue (kushoto) na wenzake, wakijifunza kutoka TARI namna ya kuweka alama wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Afisa Kilimo kutoka Wilaya ya Kongwa, Dominica Swai (kushoto) akijifunza namna ya kuweka mambo wakati wa mafunzo kwa vitendo ya upimaji wa shamba la korosho.
Mratibu wa Kitaifa wa Zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo TARI Naliendele Mtwara, Dkt.Geradina Mzena (kulia), akielekeza namna ya kunyosha mstari kwa kamba katika mafunzo hayo. 
Mkulima Richard Sanyaji kutoka Kata ya Songambele , akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba hilo la mfano la korosho la Shule ya Sekondari Mnyakongo.
Mkulima Gasper Rupia kutoka Kijiji cha Ibwaga, akijifunza namna ya kuchanganya udongo na samadi kabla ya kupanda korosho.
Afisa Kilimo kutoka Kata ya Chitego, Michael Edward, akishiriki mafunzo kwa vitendo kwa kuchimba mashimo katika shamba la mfano la korosho la Shule ya Sekondari Mnyakongo.
Mtafiti wa Kilimo kutoka Tari Naliendele, Selemani Libaburu, akitoa mafunzo ya jinsi ya kupanda korosho katika shamba la mfano la korosho la Shule ya Sekondari Mnyakongo.
Baadhi ya wananchi wa shehia ya Bumbwini wilaya ya kaskazini B Unguja waliohudhuria katika mkutano maalumu wa utowaji wa elimu dhidi ya matendo ya udhalilishaji yaliotolewa na TAMWA-Zanzibar kwa kuhirikiana na Action Aid.
Wasanii kutoa taasisi ya Thesode wakionesha igizo ambalo linaashirikia kukamatwa na mhusika wa matukio ya udhalilishaji kwa wanawake huku lengo kuu likiwa ni kutoa elimu kwa jamii kutoyafumbia macho matendo hayo.
Na Muhammed Khamis,Tamwa - Zanzibar

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa Zanzibar kwa kushirikiana na shirika la Action Aid kwa lengo la kupambana na udhalilishaji wa kijinsia wamewapatia mafunzo wanajamii 660 kutoka shehia 22 Wilaya ya Kaskazini B Unguja.

Afisa wa maswala ya udhalilishaji kutoka TAMWA-Zanzibar Zaina Salum Abdaala alisema lengo kuu la mafunzo hayo kwa wanajamii hususani wanawake ni kujengewa ufahamu zaidi juu ya dhana nzima ya udhalilishaji na madhara yake kwa kuwa bila ya kuwa na elimu sahihi dhidi ya matendo hayo hayataweza kumalizika.

Alieleza kuwa anaamini elimu hiyo ilitolewa kwa muda wa wiki mbili kwa wanajamii italeta mabadiliko makubwa ikiwemo wanajamii kufahamu viashiria vya udhalilishaji sambamba na umuhimu wa kutoa taarifa mara pale matukio hayo yanapojitokeza kwenye jamii.

Alisema kuwa katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar hadi sasa baadhi ya wanajamii wamekuwa wakiyafumbia macho matendo hayo kwa wanawake na watoto kutokana kuhofia sababu mbali mbali ikiwemo kuvunjika kwa ndoa zao.

"Kuna matukio mbali mbali ya udhalilishaji yanafanyika lakini watu wapo tayari kuona yanaendela lakini hushindwa kusema kwa kuhofia kupewa talaka na waume zao’’aliongeza.

Hata hivyo Afisa huyo aliasa jamii kubadilika na kutokuwa na muhali badala yake watoke na kutoa taarifa dhidi ya matendo hayo kwa lengo la kuchukuliwa hatua kali zaidi kwa watendaji wote watakaobainika kutenda unyama huo.

Akizungumza kwa niaba ya Masheha wenzake sheha wa shehia ya Kitope Khamis Ndende Juma alisema ni kweli kuwa wamekua wakikabiliwa na matukio mbali mbali ya udhalilishaji kwenye jamii zao kiasi cha kwamba walio wengi wameanza kushtuka na kuhofia madhara zaidi.

Alisema suala la muhali bado ni tatizo ambalo wanaendelea kukabiliana nalo ndani ya jamii zao kwa kuwa wapo baadhi ya watu wanatendewa matendo hayo na kisha kuamua kunyamaza kimya.

Hata hivyo Sheha huyo alisema kupitia elimu hio ilitolewa na TAMWA-Zanzibar anaamini kwa kiasi kikubwa itakwenda kubadili jamii na hatimae watu kuwa tayari kutoa ushirikiano wa kina dhidi ya matendo hayo kwa lengo la kuyamaliza kabisa.

Mzee Ali Makame kutoka shehia ya Kitope alisema ili jamii iweze kumaliza tatizo hilo ipo haja kuhakikisha wazazi na walezi wanakua karibu zaidi na watoto wao kila wakati.

Alisema baadhi ya matukio mengi yanayotokea yanaonesha wazi kuwa baadhi ya wazazi ama walenzi wamekosa umakini katika suala zima la uangalifu kwa watoto na wakati mwengine hua sababu ya kufanyiwa unyama huo.

Kwa upade wake Afisa Dawati la Jinsia Mkoa wa kaskazini Unguja Salum Khamis Machano alisema jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia wanajitahidi kwa kiasi kikubwa kupambana na matukio hayo ikiwemo kuwachukulia hatua wale wote wanaofikishwa katika dawati hilo.

Hata hivyo Afisa huyo alisema bado kuna tatizo ndani ya jamii ikiwemo la kukosa utayari wa kuendelea na baadhi ya kesi ambazo huwa tayari zimeshafikishwa katika vituo mbalimbali vya polisi.

Aliomba jamii kubadilika na kuyachukuliwa matendo hayo kuwa ni ya kinyama na yasiopaswa kuvumiliwa kwa mtu yoyote yule awe mzee,mtoto ndugu au jirani.