Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi akihutubia wananchi katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa wakati akifanya majumuisho ya ziara yake mkoani humo inayokwenda kwa jina la "Iringa Mpya" ambapo watedaji kutoka wilaya zote na wataalam walijumuika pamoja katika mkutano huo.

Ali Hapi amepokea kero mbalimbali za wananchi katika mkutano huo na baadhi kuzipatia ufumbuzi hapohapo kupitia watendaji wa idara mbalimbali na zingine zikichukuliwa kwa ajili ya kuchukua hatua mbalimbali za utekelezaji ili kuzitatua.

Mh. Ali Hapi amesema kampeni ya Iringa Mpya ndiyo kwaza imezinduliwa inaendelea mpaka Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli atakaposema inatosha sisi tulioaminiwa na Mh. Rais tunaendelea kutekeleza makujukumu aliyotukabidhi ili kutatua changamoto na kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika mkoa wa Iringa.

Hapi amesema ninaagiza watendaji wote kuhakikisha wanakwenda vijijini kwa wananchi ili kuwasikiliza na kutatua kero zao vinginevyo nitawapiga nyundo kabla mie sijapigwa nyundo na Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi kulia Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela katikati na MNEC wa mkoa wa Iringa CCM na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Salim Asas pamoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata wakipiga makofi katika viwanja vya Mwembetogwa Manispaa ya Iringa wakati wa mkutano wa majumuisho ya ziara ya mkoani humo ya kampeni ya Iringa Mpya leo.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela kulia na MNEC wa mkoa wa Iringa CCM na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Salim Asas katikati pamoja na Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata wakijadiliana jambo katika mkutano huo uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa mjini Richard Kasesela na msanii Bill Nas wakifanya vitu vyao katika mkutano wa Majumuisho ya Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa iliyomalizika leo iliyokuwa na kampeni ya kauli mbiu ya "Iringa Mpya".
Zuwena Mohammed 'Shilole'akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Mhe. Asia Juma Abdallah huku mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Willium akiangalia.
Zuwena Mohammed 'Shilole' akizungumza jambo na Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi pamoja na Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela huku NEC wa Mkoa wa Iringa CCM na Kamimu Mwenyekiti Ndugu Salim Asas akiangalia.
Zuwena Mohammed 'Shilole'akicheza na baadhi ya wananchi walemavu waliohudhuria katika mkutano huo.
Baadhi ya watendaji na wananchi wa mkoa wa Iringa waliohudhuria katika mkutano huo.

  
Zuwena Mohammed 'Shilole'akifanya vitu vyake mbele ya jukwaa kuu la viongozi.
Baadhi ya akina mamam wakitumbuiza katika mkutano huo.
MNEC wa mkoa wa Iringa na Kaimu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Salim Asas akitoa salam zake katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Mwembetogwa mjini Iringa leo.
Mbunge wa Viti Maalum CCM kutoka Mkoa wa Iringa Mh. Ritha Kabati akitoa salamu zake katika mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Ali Hapi ili kuzungumza na wananchi katika mkutano huo.
Steve Nyerere na Mpoki wakifanya vitu vyao kabla ya Mkuu wa mkoa wa Iringa kuhutubia mkutano huo.
Mpoki akisalimia meza kuu.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ali Hapi na viongozi wenzake meza kuu wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Picha mbalimbali zikionyesha baadhi ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: