Baadhi ya wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wakila kiapo mbele ya Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Dk. Inmi Patterson (hayupo pichani) wakati wa hafla ya kuapishwa iliyofanyika Jumatano hii, Korogwe, Tanga. Wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wa Peace Corps wapatao 59 watahudumu nchini Tanzania kwa miaka miwili katika sekta ya Elimu. Wafanyakazi hawa watapangiwa kufanya kazi katika wilaya 35 nchini kote Tanzania. Hafla hiyo ilihudhuriwa na mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha. (Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Marekani).
---
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson aliongoza hafla ya kuapishwa kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wa Peace Corps wapatao 59 watakaohudumu nchini Tanzania kwa miaka miwili katika sekta ya Elimu. Wafanyakazi hawa watapangiwa kufanyakazi katika wilaya 35 nchini kote Tanzania.Dk. Patterson aliongoza kiapo rasmi cha wafanyakazi hao wapya wa kujitolea mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.William Tate Olenasha. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi wa serikali, wafanyakazi wa kujitolea wa zamani wa Peace Corps, wawakilishi wa taasisi wabia na wanafamilia wa familia za Kitanzania ambazo wafanyakazi hawa wa kujitolewa waliishi nazo. 

Kaimu Balozi Patterson aliwaeleza wafanyakazi wapya wa kujitolea kuwa: "Wakati ambapo ninyi mnaweza kuwa Wamarekani wa kwanza kukutana na kufanya kazi na wafanyakazi wenzenu na majirani zenu wa Kitanzania, ni dhahiri kwamba katika mawazo yao mtaendelea kuwa wawakilishi wa watu wa Marekani na ubia wa muda mrefu kati ya Wamarekani na Watanzania."


Peace Corps ni taasisi ya Serikali ya Marekani iliyoanzishwa na Rais John F. Kennedy mwaka 1961 ambayo hivi sasa inahudumia zaidi ya wafanyakazi wa kujitolea zaidi ya 7,000 katika zaidi ya nchi 70 duniani. Kwa zaidi ya miaka 50, Peace Corps imekuwa taasisi inayoendesha shughuli za mabadilishano ya kiufundi na kitamaduni zisizoegemea mrengo wowote wa kisiasa na kidini. Peace Corps ina dhamira ya kukuza amani na urafiki duniani kwa kutekeleza malengo matatu yafuatayo:Kutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani watakaochangia kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika nchi itakayohitaji wafanyakazi hao:

Kukuza uelewa kuhusu Wamarekani miongoni mwa watu katika jamii zinazohudumiwa na Wafanyakazi wa kujitolea;

Kuimarisha uelewa wa Wamarekani kuhusu dunia na watu wake.

Zaidi ya wafanyakazi wa kujitolewa wa Peace Corps 3000 wamehudumu nchini Tanzania toka mwaka 1961. Peace Corps hutoa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wenye utaalamu katika nyanja mbalimbali ambao hupangiwa kufanyakazi katika jamii wakifundisha katika shule za sekondari (hisabati, sayansi na Kiingereza), wakitoa elimu ya afya na utunzaji wa mazingira.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: