Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi, Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji (katikati), wengine kutoka kushoto ni ndugu Albert Philipo, Afisa wa Wizara kutoka Idara ya Diaspora (kushoto) na ndugu Nelson Nkini, Mwenyekiti wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Msumbiji akikaribishwa katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 yanayojulikana kwa jina la FACIM yaliyofanyika tarehe 27 Agosti hadi 2 Septemba 2018 Maputo nchini Msumbiji. Ushiriki wa wafanyabiashara kutoka Tanzania uliratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Msumbiji, Mheshimiwa Carlos Agostinho do Rosário wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 ya FACIM alipotembelea banda la Tanzania na kukaribishwa na Bi. Getrude Ngweshemi, Kaimu Meneja - Masoko ya Ndani wa TanTrade na Bw. Albert Philipo, Afisa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje ambapo alipatiwa maelezo kuhusu bidhaa za viwandani pamoja na vivutio vya utalii wa Tanzania.
Balozi Rajabu Luhwavi akipokea maelezo kutoka kwa Afiisa wa Wizara, Bw. Albert Philipo kuhusu bidhaa za Tanzania zilizoletwa na wafanyabiashara mbambali kutoka Tanzania wakati wa maonesho ya biashara ya kimataifa ya 54 ya FACIM Maputo, Msumbiji. Wengine katika picha hiyo ni wafanyabiashara kutoka Kampuni mbalimbali nchini Tanzania.
Mheshimiwa Balozi Luhwavi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania walioshiriki katika Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 54 ya FACIM mjini Maputo.
Gavana wa Nampula, Mheshimiwa Victor Borges akiwa na Mheshimiwa Balozi Rajabu Luhwavi kushoto kwake wakikata utepe wakati wa kufungua Maonyesho ya Biashara Nampula tarehe 20 Agosti 2018. Maonesho hayo yalihusisha wafanyabiashara kutoka Tanzania na wenyeji wa Msumbiji.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: