Mku wa maswala ya kibiashara wa FINCA microfinance bank Emmanuel Mongella (kulia na mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa benki hiyo Nicholous John wakiongea na waadishi wa habari katika uzinduzi wa programu ya Kuza ofisi na FINCA ilioanza kuonyeshwa na TVE jijini Dar es Salaam.
---
Benki inayokua kwa kasi zaidi nchini Tanzania, Benki ya FINCA Microfinance leo imezindua shindano la runinga ambalo lina lengo la kuwaongezea uwezo wajasiriamali wadogo kwa kuwapatia stadi za biashara, ufahamu na kisha kuwapatia zaidi ya TZS Millioni 10 kwa wazo bora la biashara litakalokuwa limewasilishwa.

Awali Shindano hilo linalojulikana kama 'Kuza Ofisi na FINCA’ lilifanyika katika wilaya 4 za mkoa wa Dar es salaam, Kinondoni, Ilala, Temeke na Ubungo. Wilaya hizi zimeunganishwa kimkakati katika matawi ya benki yaliyoko Tegeta, Ilala, Victoria na kando ya barabara ya Pugu kuelekea Uwanja wa Ndege.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa program katika runinga jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya FINCA Microfinance bwana, Nicholous John amesema kwamba lengo ni kuwapatia elimu ya biashara na fedha wamiliki wa biashara ndogo ndogo ambao baadae itapelekea katika kukuza biashara zao. 

"Hii ni Hatua ya pili ya shindano ambapo washindani 8 wamechaguliwa na jopo la majaji kushiriki katika kipindi cha TV, ‘Kuza Ofisi na FINCA’ kitakachokuwa kinarushwa kupitia TVE na kuendeshwa na mtangazaji wa Efm Emamnuel Kapanga. 

Mwishoni mwa shindano, mshindi mmoja mwenye bahati ataondoka na zawadi nono ya zaidi ya TZS milioni 10", Alisema Nicholous, akiongeza kwamba washiriki wengine wenye vigezo pia watakuwa na nafasi ya kujipatia mikopo kutoka benki hiyo.

Kwa upande wake, mkuu wa maswala ya masoko wa benki ya FINCA Microfinance Benki, Emmanel Mongella amesema: "Kampeni ya Kuza Ofisi na FINCA ni sehemu ya FINCA kusherehekea miaka 20 ya uendeshaji wa shughuli zake nchini Tanzania ambapo benki ya FINCA imekuwa maarufu kwa utoaji wa masuluhisho bora na aina mbalimbali za akaunti, Mikopo na huduma zingine ambazo zinajumuisha mahitaji ya watu binafsi na taasisi."

Emmanuel pia alisema, "Ushirikishwaji wa Kifedha na Uvumbuzi wa Kidigitali ni msingi wa biashara yetu, shindano hili ni ahadi nyingine ambayo Benki ya FINCA Microfinance inatoa kwa watanzania kwamba iko kwaajili ya kuwasaidia katika misaada ya kifedha kupitia elimu na kuwawezesha wateja wetu kuweza kupata maendeleo endelevu ya biashara zao”.

Akizungumzia maono ya uzinduzi wa programu hii John alisema, “nawasii watu wote waangalie programu hii katika stesheni ya TVE maana kuna mambo mengi ya kufurahisha pamoja na elimu ya biashara”
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: