Aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush akimuongoza bintiye Barbara kwenda kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa siku nyingi Craig Coyne.
Barbara Pierce Bush akiwa na mumewe Crag Louis Coyne mara baada ya kufunga ndoa siku ya jumapili huko Maine
Picha ya familia .

Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii.

BINTI wa kwanza wa aliyekuwa Rais wa Marekani George W. Bush, Barbara Pierce Bush (36) amefunga pingu za maisha na Craig Louis Coyne (37) ambaye ni mwandishi na mtunzi wa filamu katika harusi ya siri iliyohusisha familia siku ya jumapili huko Maine.

Barbara aliongozwa na baba yake George W. Bush wakati akiolewa na Craig katika harusi ndogo iliyofanyika nyumbani kwao Kennebunkport Maine, Bush alieleza furaha yao (yeye na mkewe Laura) baada ya binti yao kufunga ndoa na kumtakia kila la heri.

Wawili hao hawakuweka mahusiano yao wazi na imekuwa harusi ya kuduwaza wengi kwani walionekana kama marafiki wa muda mrefu.

Barbara ameeleza kuwa angetamani uwepo wa bibi yake na hiyo ilikuwa zawadi kwa bibi yake na wajina wake Barbara Bush aliyefariki mwezi Aprili mwaka huu akiwa na umri wa miaka 92.

Katika ukurasa wake wa instagram bi. Laura Bush ameandika kuwa "Ilikuwa siku ya furaha kwa bintiye Barbara kufunga ndoa na mpenzi wake Craig na wamemfurahia kuwa sehemu ya familia yao" ameandika Laura kwenye picha ya familia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: