Mwenyekiti wa bodi wa Utalii Nchini (TTB) Jaji Mstaafu Maiko Miayo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana maonesho ya kimataifa ya utalii yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo (SITE) ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba Jijini Dar es Salaam.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BODI ya Utalii Nchini (TTB) imeandaa maonesho ya kimataifa ya utalii yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo (SITE) ambayo hufanyika kila mwaka mwezi Oktoba Jijini Dar es Salaam.

Lengo la maonesho hayo ni kuwaunganisha wafanyabiashara wadogo na wakati wa utalii Tanzania pamoja na wafanyabiashara kutoka masoko makuu ya Utalii.

Akizungumza na waandishiwa haari kuelekea maonesho hayo yanayotarajiwa kuanza Oktoba 12 hadi 14, Mwenyekiti wa bodi wa TTB Jaji Mstaafu Maiko Miayo amesema kuwa, onesho hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na makampuni ya uoneshaji 170 kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika na Ukanda wa bahari ya Hindi pamoja na wafanyabiashara wa kimataifa na vyombo vya habari 300.

Jaji Miayo amesema mara ya kwanza maonesho hayo yalifanyika mwaka 2014 na yalihudhuriwa na waoneshaji kutoka makampuni 40 pamoja na wafanyabiashara na vyombo vya habari va kimataifa kutoka nchi 24.

Alisema, hawakuishia hapo mwaka 2015 maonesho hayo yalizidi kuvutia na wakapokea makampuni ya utalii 110 pamoja na wafanyabiashara na vyombo vya habari 39 kutoka nchi mbalimbali duniani.

Kwa mwaka jana, onesho la SITE liliweza kuhudhuriwa na waoneshaji kutoka makampuni 145 na kufanikiwa kupata jumla ya wafanyabishara wa kimataifa na waandishi wa habari 241.

Jaji Miayo amesema kuwa, kwa mwaka huu maonesho hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa Mikutano kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC) yatakuwa yamezidi kuimariki pamoja na kuwapeleka baadhi ya washiriki katika mafunzo sehemu mbalimbali za kitalii nchini.

Wana maonesho hao wanatarajiwa kwenda katika hifadhi za Mkoani Arusha kama Hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi za Serengeti, huku kwa mkoa wa Iringa wakitembelea utalii wa kilimo na ardhi yoeru ya Mufindi pamoja na vivutio vingine vya kiutamaduni na hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Katika maeneo mengine ni Tanga, Mafia ambapo watatembelea utalii wa bahari kivuko kikuu Papa Potwe(Whale Shark), Morogoro kwenye milima ya Udzungwa na Hifadhi ya TAifa ya Mikumi pamoja na Zanzibar.

Maonesho hayo yatazidi kuboresha katika sekta ya utalii ambapo lengo kuu ikiwa ni kuongeza watalii kutoka nje ya nchi na ndani ya nchi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: