Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso akimtua mama ndoo kichwani baada ya kuzindua mradi wa majisafi Kibondemaji uliojengwa kwa ushirikiano wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) na Shirika la PDF chini ya shirika la Water Aid Nchini Tanzania. Kulia ki Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja.

Wananchi waliohudhuria uzinduzi huo.
Mbunge wa Mbagala Mhe. Ally Mangungu akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Charambe
Meneja Mradi wa Majisafi na Majitaka kutoka Shirika la PDF Mhandisi Elias Kazingoma akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso wakati wa uzinduzi wa mradi wa majisafi Kibondemaji uliofanyika leo Mbagala Charambe Jijini Dar es Salaam.

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) imetakiwa kuweka miradi ya maji pembezoni mwa miji ili wananchi wapate maji safi na salama.

Akitoa shukrani zake kwa Shirika la PDF chini ya Shirika la maji la Water Aid kwa kufanikisha miradi ya majisafi na majitaka ya Kibondemaji na Toangoma zilizopo wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Mhe. Aweso amesema kuwa  utekelezaji wa mradi huo ni katika kukabiliana na changamoto ya ukuaji wa watu kwa haraka katika miji na lengo kuu ni kuona 2020 asilimia 95 wananchi wanapata maji safi na salama ya uhakika.

Aweso amesema kuwa, kuna miradi 12 ya maji ya visima virefu vinavyojengwa katika Manispaa ya Temeke inayojengwa ikiwemo na mradi wa majitaka na vyoo vya umma uliochini ya Benki ya umma.

"Nawaomba DAWASA mzidi kusisitiza miradi mingi iende pembezoni mwa mji maana huko ndipo wananchi wanataabika na kukosa maji safi na salama," amesema Aweso.

Nae  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja kukamilika kwa mradi wa Kimbiji Mpera utaweza kuondoa changamoto kubwa ya maji pembezoni mwa Mji ambap kufikia Desemba mkandarasi atawakabidhi visima vinane.

Luhemeja amesema kuwa, tayari ana Bilioni 3 mkononi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa miundo mbinu ya maji na kupitia mapato ya DAWASA wametenga asilimi 35 kwa ajili ya kuweka miundo mbinu kwenye maeneo tofauti ikiwemo Kipawa kuelekea Buza, Kibamba , Kisarawe hadi Pugu.

Mradi wa Majisafi uliopo kata ya Kibondemaji na Charambe unalenga kuhakikisha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wakazi wa mitaa ya Kibondemajj A na kurasini mji mpya kata ya Charambe watakaonufaika na mradi huo.

Mradi wa maji Kibondemaji -Charambe utahudumia mitaa minne ambayo ni mtaa wa Kibondemaji A, majimatitu C , Mchikichini na Kimbangulile pamoja na Mtaa wa Kurasini Mjimpya uliopo kata ya Charambe.

Mradi wa Majisafi una jumla ya urefu wa Kilometa 11 na kisima chenye urefu wa mita 180 chenye uwezo wa kutoa maji kiasi cha Lita 224,000 kwa siku ikijumuisha vibanda 7 vya kuchotea maji (water Kiosks).

Gharama ya mradi wa Majisafi ni Milioni 187 za Kitanzania ukiwa na malengo ya kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa kata ya Kibondemaji, mbali na hilo pia kuwajengea uwezo wa kibiashara wajasiriamali wadogo wa shughuli za usafi wa mazingira.

Pia mradi huo utasaidia upatikanaji wa huduma za udhibti wa majitaka kwa wakazi wa kata za Kibondemaji, mianzini, Charambe, Kiburugwa na Kulingule.

Shirika PDF chini ya Shirika lla WaterAid limetumia kiasi cha Milioni 547.4 kwa miradi ya Majisafi na Majitaka na kwa pamoja wamesaini mkataba maalumu unaompa mamlaka kamili ya usimamizi wa mradi huo kwa DAWASA.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: