Msanii Bonta Maarifa akitoa burudani katika Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote iliyofanyika Musoma.
Msanii Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q akiwa kwenye jukwaa la Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Karume mjini Musoma usiku wa kuamkia jumatatu.

Wasanii Fid Q na Jux usiku wa kuamkia jana waliacha alama ya Vibe la Tigo Fiesta kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma.

Wasanii hao kwa wakati tofauti wakiwa kwenye steji waliweza kuteka hisia za mashabiki waliofurika uwanjani hapo. Msanii Fid Q ndiye aliyefungua pazia la Tigo Fiesta mjini Musoma mkoani Mara, Kwa mkoa huo wasanii wanaopendwa zaidi ni wa mtindo wa kufokafoka (Hip Hop) ndipo Fid Q alipopewa jukumu la kuanza na kuamsha shangwe kubwa na hasa alipomaliza kwa wimbo wake ujulikanao kama FRESH.
 Nae Juma Jux ambaye ni "Fundi" wa nyimbo Laini aliweza kuwaimbisha mashabiki mwanzo hadi mwisho aliposhuka kwenye jukwaa hilo kwa nyimbo zake JUU, ZAIDI na UTANIUWA na nyingine nyingi kwa kweli huyu ndio msanii aliyeweza kuimba na mashabiki kwa pamoja.

Tamasha hilo linatarajiwa kuendelea mjini Muleba ijumaa hii kwenye uwanja wa Zimbihire.
Mwisho.
 Msanii Richie Mavoko akitoa burudani.
 Wasanii wa Nchama The Best wakitoa burudani.
 Msanii Nedy Music akitoa burudani.
Wakazi wa mji wa Musoma wakifuatilia kwa makini Tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: