Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kote nchini kumtakia heri ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.

Ni Oktoba 29, 1959 ni siku ambayo Mwenyezi Mungu alitupa Watanzania zawadi ya Mtoto John Pombe Magufuli ambaye Leo hii amekuwa lulu, Mkombozi, Shujaa, Mtetezi, Mlezi, Mjenzi wa Watanzania. Leo hii ni nembo ya uongozi wa mfano Afrika na Duniani kote.

Dkt. Magufuli ametumia nguvu na akili zake zote kuhakikisha mitandao ya Barabara, Madaraja yanajengwa nchi nzima na Leo anajenga Reli ya kisasa ya umeme kwa kiwango cha standard gauge pasipo kusahau kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania kwa kununua ndege mpya saba.

Kwa kupitia uzalendo na uchapakazi wake Leo hii elimu inatolewa bure nchi nzima; rushwa na ufisadi anavipiga vita kwa vitendo; rasilimali za Taifa anahakikisha zinalindwa vilivyo ili kumnufaisha Mtanzania n.k.

Kwa ufupi maisha yake yamekuwa ya msaada mkubwa kwa Watanzania kwani ameonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na Maadui zetu ambao ni ujinga, maradhi na umaskini.

Pia ameonyesha mapenzi ya dhati ya kusimama upande wao Watanzania Wanyonge yaani Wakulima, Wafanyakazi, Wavuvi na Wafugaji kote nchini. Watanzania wanyonge hawana la kukulipa zaidi ya kukutakia Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu yenye baraka tele, uendelee kuwatumika vyema Watanzania.

Heri ya Kuzaliwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Shilatu E.J
0767488622
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: