mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Kalist Lazaro akitoa maelezo kwa waandishi wa habari hawapo pichani ofisini kwake jijini Arusha wakati akitoa maelezo ya maonyesho ya kimataifa yatakayofanyika jumamosi ya Tarehe tatu mwaka huu picha na Mahamoud Ahmad Arusha.

Ahmed Mahmoud, Arusha.

Wananchi wa jiji la Arusha wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na mashirika ya kimataifa yanayofanyakazi ndani ya jiji hilo lengo likiwa ni kuangalia fursa zinazotokana na mashirika hayo kukuza vipato vyao na uchumi wa jiji hilo.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha Mstahiki Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro amebainisha kuwa Maonyesho hayo Pili ya mashirikia ya kimataifa yanayojulikana kwa jina la (Internation Organization Arusha open day)yanatarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 3 mwezi novemba katika viwanja vya lakilaki nje kidogo ya jiji la Arusha.

Amesema kuwa wananchi watatakiwa kuwa na vitambulisho kuweza kushiriki maonyesho hayo ambayo ni mara ya pili yanafanyika na mgeni rasmi atakuwa Waziri wa mambo ya nje kikanda na Afrika mashariki Balozi Agastine Mahiga na usafiri utakuwepo maeneo yote ya jiji hili na kiingilio ni bure

Amesema kuwa maonyesho hayo ambayo yanafanyika katika majiji matatu tu ya Durban New York na Arusha mwakani kitaifa yatafanyika jijini Dar es salaam na hivyo kutoa fursa kwa taasisi mbali mbali za kimataifa ambazo zipo hapa nchini kuweza kushirikiana na wananchi katika kuonyesha shughuli wanazozifanya hapa nchini lengo likiwa ni wananchi kujua shughuli wanzozifanya na fursa gani wanaweza kushirikiana.

Amesema kuwa maonyesho hayo ambayo mwaka jana yalikuwa ya majaribio hivyo kuwataka wananchi wengi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika maonyesho hayo ikiwa ni sehemu ya kukutana na kuweza kujua mashirika hayo yanafanya nini na yapo eneo gani kuweza kujua fursa walizonazo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: