Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu (kushoto), akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, kwenye jukwaa la TEF wakichambua kuhusu hali uchumi na umuhimu wa vijana Afrika kuwa wabunifu jijini Lagos, Nigeria
 Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu (kushoto), akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, wakiwa na kijana mshiriki wa kongamano kutoka nchini Ghana baada ya kijana huyu kutaka ufafanuzi kwa Rais wake wa namna vijana wanavyopewa kipaumbele katika ujenzi wa uchumi wa nchi hiyo.
 Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu, akiwa na Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo, wakiwa watendaji wa Taasisi wa Tony Emelu Foundation wakati wa uzinduzi wa tovuti ya taasisi hiyo jijini Lagos, Nigeria
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika wakiwa kwenye majadiliano wa maofisa Uhusiano wa Benki za UBA, jijini Lagos
Mshiriki wa kutoka Tanzania, Kinshaga akionesha bidhaa kwa washiriki wa jukwaa la TEF jijini Lagos, Nigeria.

Na MWANDISHI WETU - Lagos, Nigeria.

MARAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya na Nana Akufo-Addo wa Ghana wamewataka vijana Bara la Afrika kuwa wabunifu na kumchangamkia fursa za kiuchumi ili kuiweza kusaidia nchini zao.

Kauli hizo wametoa hivi karibuni jijini Lagos nchini Nigeria kwenye jukwaa la nne la kila mwaka lililoandaliwa na Taasisi ya Tony maarufu Tony Elumelu Foundation (TEF), Entrepeneurship Forum.

Rais Uhuru Kenyatta, aliwahimiza vijana kutoka bara la Afrika kutumia ubunifu wao ili kuleta mabadiliko.

“Viongozi vijana wabunifu kutoka Afrika wanapigana na mabadiliko yenye nia njema kwa kutumia teknolojia. Kuwa bora iwezekanavyo kwa familia, jamii, taifa yako lakini muhimu wewe mwenyewe,” amesema

Rais Uhuru alisisitiza ushauri wake kwa vijana kufanya kazi ili kuwa bora kwa taaluma ambayo wamechagua.

Tukio hilo ni fursa pekee ya kukusanya vipaji vya biashara kwa vijana, kujenga mitandao yenye nguvu na kupeleka ujumbe kwa watunga sera kwamba sekta binafsi iliyo mahiri na inawajibika inauwezo wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi.

Baada ya kupata mafunzo ya miezi tisa, ushauri na ufadhili, jumla ya vijana 4,470 walifaidika na programu hiyo iliyoshuhudia zaidi ya vijana laki tatu wakituma maombi.

Mwasisi wa jukwaa hilo, Tony Elumelu, alisisitiza kuendelea kujitolea kuhakikisha maendeleo ya uchumi Afrika kwa kusaidia mafunzo ya kizazi kipya cha wajasiriamali ambao mafanikio yao yanaweza yakabadili bara hili ikwemo kutengeneza ajira.

“Ujasiriamali ni muhimu kufungua maendeleo ya uchumi katika bara letu. Naamini kwa dhati mafanikio yanaweza yakaleta demokrasia na kama tunaweza kubadili tamaa na kuwa fursa, hiki kizazi cha ajabu kinaweza kufanikiwa kwa kila jambo,” alisema Tony Elumelu

Naye Rais wa Ghana, Nana Akudo-Addo, aliwasisitizia wawakilishi wa sekta ya umma kuhimiza, kusaidia na kuiga kazi inayofanywa na Taasisi ya Tony Elumelu.

“Hakuna kinachobadilika au kujiendeleza kivyake. Watu lazima waamke, waonge, wajadili na kubadilisha mada,” alisema Rais Nana Akufo-Addo.

Tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo, imeweza kuwasaidia wajasiriamali Waafrika kutoka pembe zote za Bara la Afrika na washindi katika mashindano mbalimbali katika jukwaa la mwaka huu walipata ufadhili wa dola za Marekani 5000 (takribani Shilingi milioni 11.4 kila mmoja).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: