Muandaaji wa Muziki nchini Tanzania, Producer Pancho Latino almaarufu Mafia (Pichani) ambae alifanya kazi kwenye studio mbalimbali  aliyefariki jana kwa  kuzama kwenye maji kwenye kisiwa cha Mbudya Dar es Salaam anatarajia kuzikwa Wilayani Gairo, Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa na Msanii Fid Q katika ukurasa wake wa Twitter imesema kuwa Marehemu  Pancho Latino itahitimishwa siku ya Jumamosi Oktoba 13, 2018 nyumbani kwao.

Ibada itaanza saa 4 asubuhi, na baadae wataaga mwili wa marehemu na maziko yatafanyika saa nane mchana.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Lugalo kwa uchunguzi zaidi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: