Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akisaliana na Bibi Aisha Hamisi wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Kiomboi Wilayani Iramba Mkoani Singida kuangalia hali ya utoaji wa huduma za Afya, Ustawi na Maendeleo ya Jamii.

Na Mwandishi Wetu Singida.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi kuhakikisha Bibi. Aisha Hamisi aliyeishi zaidi ya miaka kumi katika Hospitali ya Kiomboi iliyopo Wilaya ya Iramba Mkoani Singida anapelekwa katika Makao ya kuhudumia Wazee na Wasiojiweza.

Hatua hiyo imekuja baada ya Naibu Waziri huyo kuongea na Mzee huyo na kupata taarifa kuwa hana ndugu wala Jamaa wa kumlea hivyo anakosa huduma muhimu za kibinadamu wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Kiomboi iliyopo Wilaya ya Iramba Mkoani Singida.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya ya Iramba amemueleza Naibu Waziri Ndugulile kuwa Bibi Aisha Hamisi amekaa zaidi ya miaka kumi katika Hospitali ya Kiomboi alikuwa akitibiwa na kuendelea kukaa hapo kwa kukosa ndugu wa kumchukua na kumtunza.

Aidha Dkt. Ndugulile ameagiza Mzee huyo apelekwe katika Makao ya kuwahudumia Wazee na Wasiojiweza ya Sukamahela yaliyopo Wilaya ya Manyoni ili kupata huduma muhimu.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Serikali ina jukumu la kuwatunza Wazee na Wasiojiweza kwa wale ambao hawana ndugu wala jamaa wa kuwatunza.

Akipokea maelekezo hayo Kamishna Msaidizi wa Ustawi wa Jamii Bw. Rabikira Mushi amesema kuwa suala la kumuhamishia Bibi Aisha kwenye Makao ya Wazee litafanyika mara moja na hatahamishiwa katika Makao ya Wazee ya Sukamahela.

Kwa upande wake Bibi Aisha Hamisi amemshukuru Naibu Waziri kwa kuja kutembelea Hospitali ya Kiomboi na kumwomba kutatua changamoto za matibabu zinazowapata Wazee.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: