Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed akizungumza wakati wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora akitoa mada ya Umuhimu wa Taifa huru na uhuru wa Wananchi katika kukuza uchumi wa Viwanda.
Mkuu wa Wilaya ya Kigambboni Sarah Msafiri akizungumza kuhitimishaKongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere.
CAG Mstaafu, Ludovick Utouh akichangia mada katika Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.
Watoa mada na Wajumbe wa Meza kuu wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.
Viongozi wastaafu na wadau mbalimbali wakifatilia kwa karibu Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wakifatilia kwa makini Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.
Picha ya Washiriki wa Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere Lililofanyika katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kampasi ya Kivukoni Dar es Salaam.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Mohamed Ali Ahmed ametaka kutungwa kwa sheria Maalum kwa watu watakaobeza Muungano kutajwa kuwa ni wahaini.

Ahmed amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akichangia Mada katika kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere lililobebwa na Mada ya ‘Falsafa ya Mwalimu Nyerere juu ya Kujitegemea na Maendeleo ya Viwanda Tanzania’.

“Mimi ninachoomba tuvutane tu ila tuwandalie mstakabali mzuri hao wanakuja nyuma yetu na tuwajenge hawa kwa mazuri nimeguswa kidogo na katibu wa baba wa Taifa pale alipouliza nyie vipi huko katika vyama vya siasa nimekuwa nashangaa sana wanasiasa awajui kupambanua kipi cha kubeza na kipi sio cha kubeza”

Ahmed amesema kuwa kuna tatizo la kisheria katika mfumo wa kuongoza hivi vyama kwani wanasiasa ndio wamekuwa kipaumbele kuhoji muungano jambo ambalo linafanywa kwa utashi wa kulenga kupata kura tu.

Amesema ifike wakati wakusema kuwa mtu akigusa Muungano ni uhaini sio kwa kumgusa Rais Peke
yake kwani wanfanya hivi kwa kutaka kupata umaharufu wa kisiasa.

Amesema ifike mahali ni sharia kufata fikra za Mwalimu kwani anayekiuka hizo atakuwa ametendakosa kubwa la jinai kwani tukiacha uhuru tutaendelea kudanganyana siku hadi siku.

Alimaliza kwa kusema kuwa leo amekuja Rais Dk John Magufuli anasimamia haya lakini ipo siku atakuja kiongozi atayaaopuuza haya anayofanya kisha taifa hili litapromoka kwa kiwango cha ajabu nakupoteza nguvu yote hii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: