Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga akisalimiana na mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Rukwa wakati alipowasili katika eneo la kutundika mizinga katika manzuki ya Nawima iliyoko katika Msitu wa Mto Kalambo katika mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo (kushoto) akisoma taarifa ya ufugaji nyuki katika mkoa wake mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga
Baadhi ya wananchi wakipunga mikono kwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya utundikaji mizinga iliyofanyika kitaifa mkoani Rukwa katika manzuki ya Nawima iliyoko katika Msitu wa Mto Kalambo
Mtendaji Mkuu waTFS Prof. Dos Santos Silayo akitundika mzinga katika maadhimisho ya Kitaifa ya utundikaji mizinga ya nyuki ambapo jumla ya mizinga 100 imetundikwa leo katika manzuki ya Nawima iliyoko katika Msitu wa Mto Kalambo katika mkoa wa Rukwa.
Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Mhe. Joachim Wangabo (wa tatu kulia) akiwa na baadhi wa viongozi walioshiriki maadhimisho ya Kitaifa ya utundikaji mizinga ya nyuki ambapo jumla ya mizinga 100 imetundikwa leo katika manzuki ya Nawima iliyoko katika Msitu wa Mto Kalambo katika mkoa wa Rukwa
Baadhi ya mizinga 100 iliyotundikwa katika maadhimisho ya kitaifa ya utundikaji mizinga iliyofanyika katika manzuki ya Nawima iliyoko katika Msitu wa Mto Kalambo katika mkoa wa Rukwa
Baadhi ya wanafunzi wa shule za misingi waliohudhuria maadhimisho ya utundikaji mizinga iliyofanyika kitaifa mkoani Rukwa katika manzuki ya Nawima iliyoko katika Msitu wa Mto Kalambo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga azindua utundikaji mizinga katika mkoa wa Rukwa. (PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: