Mjumbe wa Tamasha la Tigo Fiesta toka Clouds Media, Hamisi Mandi Maarufu kama B12 (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Moshi jinsi tamasha hilo litakalofanyika kesho uwanja wa Majengo mjini Moshi kuwa litakuwa lenye ubora wa hali ya juu. Wengine pichani toka kushoto ni Mr. Blue, Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka, Rosa Ree na Kennedy The Lemedy.
Msanii Rapa wa Kike Tanzania, Rosa Ree akizungumza na wanahabari kwenye hoteli ya Panama leo mjini Moshi.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jinsi wapenzi wote wa muziki mjini Moshi watakavyofurahia promosheni tatu murwa katika msimu huu wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Pembeni yake kutoka kushoto ni Hamisi Mandi B12, Mr. Blue, Rosa Ree na Kennedy The Lemedy.
Tigo Fiesta 2018- Vibe Kama Lote imewasili mjini Moshi na ahadi ya kuwapagawisha mashabiki wa muziki kwa vibe asilimia 100% za nyumbani pamoja na promosheni tatu kabambe zitakazoendana na fursa kubwa za kibiashara kwa wakaazi wote wa mji huo.

Mdhamini mkuu wa msimu huu wa Tigo Fiesta 2018, kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Moshi kufurahia promosheni zake tatu murwa katika msimu huu wa vibes. ‘Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Kaskazini, Nancy Bagaka alisema.

Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Kwa tamasha la Moshi litakalofanyika katika viwanja vya Majengo, tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa Tigo Pesa Masterpass QR zitagharimu TSH 8,000 pekee badala ya TSH 10,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslim, Wateja wanapaswa kupiga *150*01# na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Masterpass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.

Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za TSH 100,000, zawadi za kila wiki za TSH 1 milioni, simu janja za mkononi zenye thamani ya TSH 500,000 kila moja, pamoja na donge nono la TSH milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz na kuchagua Trivia.

Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu linashirikisha 100% wasanii wa nyumbani wanaozuru mikoa 15 ya nchi ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: