Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwakabidhi Shilingi milioni 50, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe pamoja na viongozi wa TFF ili zitumuke katika maandalizi ya mechi inayokuja ya kuwania kufuzi AFCON nchini Cameroon. Wengine katika picha ni Rais wa TFF Wallace Karia, Katibu Mkuu wa TFF Wilfred Kidao pamoja na Nahodha wa Timu ya Taifa Erasto Nyoni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo mara baada ya kukabidhi Shilingi milioni 50 kwa TFF kwa ajili ya Maandalizi ya Timu ya Taifa Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Ikulu.
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametoa shilingi Milioni 50 kwa timu ya Taifa ya Tanzania.

Fedha hizo ni kwa ajili ya safari ya mchezo wa marudiano baina ya Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dhidi ya Lesotho utakaochezwa Novemba 16, mwaka huu. 

Akiwa anazungumza na wachezaji na viongozi katika hafla ya chakula cha Mchana Ikulu Jijini Dar es Salaam, Dkt Magufuli amesema kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya safari na sio kwa wasindikizaji.

“Nawapa Millioni 50 kwa ajili ya safari ya Lesotho, fedha hizi zitumike kwa ajili ya wanaotakiwa kusafiri tu, sio mambo ya wachezaji 15, viongozi wasindikazaji 30. Haya mambo yafikie mwisho.” amesema Dkt Magufuli.

Mbali na hilo amewataka wachezaji kujituma na kuacha mambo ya kihuni, "Wachezaji wasipoacha uhuni watakuwa wanafunga magoli mengine ila ya uwanjani watashindwa"

Taifa Stars katika mchezo uliopita dhidi ya Cape Verde walifanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 2-0 mechi iliyopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa na kufikisha jumla ya alama 5 akishika nafasi ya pili nyuma ya Uganda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: