Mwalimu Mwakasege (Pichani kulia) akiwa na Mtoto wake Joshua ambaye kwa sasa ni Marehemu.

Ratiba ya Kumuaga mtoto wa Mwalimu Mwakasege aliyefariki Alhamisi Oktoba 11 :- Mwalimu atawasili Dar es Salaam Jumatatu. Jumanne mwili utaagwa Mbezi Beach Lutheran Church, Jumatano alfajiri ni safari kuelekea Mbeya, na Alhamisi ni mazishi mjini Tukuyu Wilayani Rungwe Mkoani Mbeya.

Mahali ulipo msiba: - Msiba uko Dar es Salaam kwa mdogo wake Mwalimu Mwakasege anaitwa Eng. Mwakasingila (Mzee wa kanisa wa KKKT Mbezi Beach).  

Jinsi ya kufika msibani Fika hadi Mbezi Beach Jogoo, unaingia barabara ya Karibu Art Gallery kuelekea TAG Mbezi Beach kisha utaona vibao vinavyoelekeza msiba ulipo. 

Ratiba ya Jumatatu Kutakuwa na sara ya pamoja na Mwalimu Mwakasege na familia yeke yote itakayofanyikia hapa msibani itakayoanza saa moja jioni, 7pm itakayoongozwa na Askofu Mchungaji kiongozi na watumishi wengine.

Kuaga Mwili wa marehemu utaagwa Jumanne 16 Oktoba kanisani KKKT Mbezi Beach Dar es , kuanzia saa nane mchana (2pm) Baada ya kuaga mwili utapelekwa airport kwa ajili ya maandalizi ya safari. 

Kusafirisha: Mwili utasafirishwa Jumatano 17 Oktoba kwa ndege Mazishi: Yatafanyika alhamisi, Tukuyu, Mbeya 18 Oktoba, 2018. 

Muhtasari: Joshua amefariki ghafla baada ya kudondoka alhamisi tarehe 11 Oct 2018 akiwa kazini kwake World Bank Dar. Alikimbizwa Aga Khan hospital ila alifariki siku hiyo hiyo.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMEN.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: