Na Ahmed Mahmoud, Arusha.

Shirika la Hand in Hand Eastern Afrika, linalojihusisha na utoaji wa mafunzo ya ujasirimali ,limegawa miti ya kivuli 150 katika shule ya sekondari ya Losurway na Ngarenaro zilizopo katika jiji la Arusha kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi kutunza mazingira.

Akizungumza wakati wa kupanda miti hiyo, Meneja wa tawi la Arusha kutoka shirika hilo, Jane Sabuni alisema kuwa, wamefikia hatua ya kutoa miti hiyo Kwa shule hizo kutokana na kuwepo kwa ukame mkubwa katika shule hizo na wanafunzi kukosa sehemu ya kupumzika.

Jane alisema kuwa, shirika hilo limekuwa likitoa elimu ya utunzaji wa mazingira na upandaji miti ambapo wanafanya kazi na baadhi ya vikundi mbalimbali vya wajasiriamali ambapo huwahamasisha kupanda miti hiyo kwa ajili ya kivuli na biashara pia .

“Sisi kama wadau wa mazingira tumeanzia na shule hizi zilizopo pembezoni ambazo zinakabiliwa na changamoto ya ukame na mmonyoko wa udongo kutokana na ukosefu wa miti, hivyo baada ya hapo tutaenda shule zingine zilizopo pembezoni zinazokabiliwa na changamoto Kama hii. “alisema Jane.

Alisema kuwa, wamefikia hatua ya kuanzia mashuleni ikiwa ni mojawapo ya harakati za kuwahamasisha wanafunzi hao kupenda kutunza mazingira wakiwa tangu wadogo ili wakawe mabalozi katika maeneo yao mbalimbali.

Naye Mkuu wa shule ya Losurway, Bertha John alisema kuwa, shule hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya mmonyoko wa udongo na kivuli kutokana na ukosefu wa miti ,hivyo uwepo wa miti hiyo utasaidia sana utunzaji wa mazingira.

Alisema kuwa, msaada huo umekuja Kwa muda muafaka ambao walikuwa na uhitaji mkubwa wa miti ya kivuli ambayo itawawezesha wanafunzi kupumzika na kujisomea hasa kipindi cha mitihani.

Mmoja wa wanafunzi shuleni hapo , Valentine Jackson alisema kuwa,uwepo wa miti hiyo ya kivuli itasaidia Sana kuondoa msongamano wa wanafunzi wakati wa mitihani ambapo huwalazimu wanafunzi hao kusimama kibarazani wakisubiri wenzao wamalize mitihani huku wanafunzi hao wakiahidi kuitunza kwa bidii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: