Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Rehema Abdalah ambaye amekuwa akiishi karibu na kisima ambacho kiligunduliwa na Wajerumani mnamo karne ya 15 . Maji ya kisima hicho hutumika katika kufanya matambiko kwa wenyeji wa maeneo hayo na pia watu mbalimbali wamekuwa wakifika na kuchota maji katika kisima na kuyanawa wakiamini kuwa ni dawa na yamekuwa yakito mikosi. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Rehema Abdalah ambaye amekuwa akiishi karibu na kisima ambacho kiligunduliwa na Wajerumani mnamo karne ya 15 . Maji ya kisima hicho hutumika katika kufanya matambiko kwa wenyeji wa maeneo hayo na pia watu mbalimbali wamekuwa wakifika na kuchota maji katika kisima na kuyanawa wakiamini kuwa ni dawa na yamekuwa yakito mikosi. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni ,maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akipewa maelezo na Mzee Mohamedi Kidume kuhusiana na Nyumba aliyofikia na kulala aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika nyumba hiyo ambayo kwa sasa imekuwa gofu. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni maadhimisho ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini.
Baadhi ya maandishi yanayoonesha kuwa Mji Mkongwe wa Mikindani umetangzwa rasmi kwenye gazeti la serikali, Mji huo utafungua milango ya watlii kwa mikoa ya Kusini.
Baadhi wananchi wakimskiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizindua Mji Mkongwe wa Mikindani ambao umetangazwa kuwa ni kituo cha Urithi wa Taifa na kivutio cha Utalii
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga (wa tatu kushoto) akipewa maelezo na Meneja Mradi wa Trade Aid,Emmanuel Mwambie( wapili kushoto) kuhusiana na ukarabati wa Old Boma la ambayo kwa sasa inatumika kama hoteli na pia kama kituo cha kufundishi vijana zaidi ya 400 kuhusiana na kozi ya ukarimu kwa watalii. Naibu Waziri huyo ametembelea eneo hilo ikiwa ni siku ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania pamoja na Siku ya Mikindani lengo likiwa ni kuenzi na kutunza mji huo ambao ni lango la utalii wa mambokale kwa mikoa ya Kusini. Wanne kulia ni Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Monica Mussa

( PICHA ZOTE NA LUSUNGU HELELA-WMU)

Wizara ya Maliasili na Utalii imeagizwa ishirikiane na wadau wa utalii wenye nia ya kuwekeza kwenye majengo na maeneo ya kihistoria yaliyopo nchini kwa kuboresha hali ya majengo hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu zaidi na yaendelee kutumika kama kivutio cha Utalii.

Pia, Wizara hiyo imeagizwa ianze mara moja ukarabati wa jengo ambalo Mwl.Nyerere alifikia na kulala kwa muda wa siku mbili wakati wa harakati za kupigania uhuru kutoka kwa wakoloni.

Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga wakati kisoma hotuba kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa katika maadhimisho ya siku ya tamasha la urithi wa Mtanzania na siku ya Mikindani iliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mhe. Hasunga ameutangaza mji Mkongwe wa Mikindani kuwa ni kivutio rasmi cha Urithi wa Utamaduni na Malikale hapa nchini kufuatia kuhifadhiwa kwake rasmi kisheria kwa tangazo la Serikali namba 308 la mwezi Julai mwaka huu.

Kufutia juhudi hizo za Serikali za kutaka kuongeza idadi ya watalii,Waziri huyo amesema juhudi hizo zitasaidia kutangaza na kuhamasisha jamii kupenda na kuenzi utamaduni wao na hivyo kuulinda na kuutumia utamaduni kama fursa ya kukuza utalii kwa mikoa ya kusini.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema tamasha hilo limekuwa muhimu kwa Wanamtwara kwa vile linafungua milango kwa watu binfasi pamoja na Mashirika kuwekeza kwenye utalii wa mambokale.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa utalii wa ukanda wa kusini hali itakayopelekea majengo mengi ambayo yamechakaa sana yaweza kukarabatiwa baadala ya kutegemea Wizara pekee.

Kwa upande wake, Kaimu Naibu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andy Karas, ameipongeza Serikali kwa hatua inazozichukua za kuhakikisha maeneo yenye historia yanatunzwa na kuenziwa.

Mji mkongwe wa Mikindani ni mojawapo ya maeneo yenye majengo mengi mazuri ya kihistoria yaliyojengwa karne ya 15 na 19 wakati wa utawala wa kikoloni hapa nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: