Tunafahamu kuwa serikali yetu ina utashi mzuri wa kisiasa kwa kuwekeza nguvu kubwa katika ges, ila bado kuna changamoto kubwa katika ges hiyo kwa wananchi kushindwa kumudu gharama zake hivyo kusababisha wananchi hao kuendelea na matumizi ya nishati ya mkaa na Kuni kama nishati mbadala.
Muwezeshaji na mtaalam wa mambo ya jinsia Geofrey Chambua akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo wadau kutoka vituo vya taarifa na maarifa Morogoro pamoja na Shinyanga.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es salaam na Ndugu Geofrey Chambua ambaye ni mchambuzi wa maswala ya jinsia hapa nchini katika semina ya kuwajengea uwezo wanachama wa Vituo vya Taarifa na Maarifa kutoka mkoa wa Morogoro pamoja na Shinyanga. 

Semina hiyo ya siku mbili iliyofanyika tarehe 25 na 26 mwezi septemba huku lengo kuu likiwa ni kujadili changamoto za ufikiwaji wa rasilimali ya nishati ya gesi pamoja na umeme katika mlengo wa kijinsia, na imehusisha wadau kutoka kata za Kibuka na Bwakira chini mkoani Morogoro, Maganzo na Ukenyenge mkoani Shinyanga.

Chambua alisema kuwa serikali imetoa pesa nyingi sana katika kuendeleza miradi mikubwa ya umeme kama Stiegler`s Gorge na umeme wa gesi lakini umeme huu usipofika maeneo ya vijijini bado utampa mzigo mkubwa mwananchi wa chini hususani mwanamke kwa kuendelea na matumizi ya nishati mbadala ya mkaa pamoja na kuni.
Bi. Kabula Lindima kutoka kata ya Maganzo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga akielezea hali halisi kwa mkoa wao kuhusiana na matumizi ya nishati ya gesi na umeme.

Aliendelea kusema kuwa katika mapinduzi ya uchumi wa viwanda na kuelekea katika nchi ya uchumi wa kati kundi la wanawake na wasichana wasiachwe nyuma kwani takwimu zinaonyesha kuwa asilimia zaidi ya 70 ya nishati inatumika nyumbani na watumiaji wakubwa ni kundi hili la wanawake na wasichana na sio kundi lingine.

Pia alisisitiza kuwa kundi hili la wanawake na watoto wa kike bado limeendelea kuwekwa chini hata katika ngazi za maamuzi, Kwani washiriki wamebainisha kuwepo na uminywaji wa demokrasia kwa kundi hili, Na hii ni kutokana na uchache wao katika ngazi za maamuzi na kusababisha kukosa watu wa kuzizungumzia changamoto zao, lakini pia sera na mipango ya nchi haikuakisi katika kumkomboa mwanamke kwa upande wa nishati hii. 

Kwa upande wake Bi. Kabula Lindima kutoka kata ya Maganzo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga alisema kuwa nishati ya umeme katika eneo lao bado ni changamoto japokuwa wamezungukwa na Mgodi wa Nyamongo, lakini shule na maeneo mengi ya karibu hakuna nishati hii hali inayofanya wanafunzi na wakazi wa maeneo hayo kutumia nguvu kubwa katika kutimiza majukumu yao endapo yanahitaji nishati hiyo.
Semina ikiendelea
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: