Na Woinde Shizza, Arusha.

Vijana nchini wametakiwa kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ambayo imekua ikitumika kufanya uhalifu wa kimtandao pamoja na kuchangia kuporomoka kwa maadili ya vijana wanaoiga tamaduni za nchi za nje zisizofaa.

Akizungumza katika Kongamano la Maadili liliofanyika Wilaya ya Karatu ,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Arusha Dk. John Pallangyo amesema kuwa vijana wanapaswa kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao pamoja na kuhakikisha kuwa wanalinda maadili ya Tanzania na kuchangia maendeleo kwenye jamii na taifa.

Dk.John alisema kuwa vijana wanatakiwa kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa na kujiongezea maarifa sahihi pamoja na kukuza kipato badala ya kutumia katika mambo yasiyofaa.

Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Karatu Peter Mmasy amesema kuwa jumuiya hiyo ina jukumu la kusimamia malezi,maadili ya jamii na kuwataka Wazazi kutimiza wajibu wao kwa kuwalea vyema vijana.

Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa mkoa wa Arusha kupitia CCM, Cylius Daniel Mlekwa amesema kuwa licha ya kusisitiza maadili pia vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupiga vita rushwa ili kuwa na jamii bora.

Cylius alisema kuwa vijana nchini waunge mkono juhudi za kupambana na rushwa katika kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinalindwa kama anavyofanya Raisi John Magufuli.

Kwa Upande wake Kijana aliyeshiriki katika Kongamano hilo Elitumaini Rweyemamu amesema maadili na nidhamu ni nguzo ya mafanikio kwa vijana hivyo vijana hawana budi kusimamia vyema maadili ya kitanzania ambayo yamegubikwa na utandawazi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: