Vijana wa Kata ya Kunduchi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwenda kuchukua mikopo iliyotengwa na halmashauri, kwani ni haki yao ya msingi na ni agizo kwa kila halmashauri kuweza kutenga asilimia nne kwa vijana, asilimia nne kwa wakina mama na asilimia mbili kwa ajili ya walemavu.

Rai hiyo imetolewa jana eneo la Kunduchi jijini Dar es salaam na Katibu wa Idara ya Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Taifa Bw. Hassan Bomboko alipokuwa mgeni rasmi katika Bonanza la Vijana lililoandaliwa na UVCCM kata ya Kunduchi.
Katibu wa Idara ya Hamasa na Chipukizi wa UVCCM Taifa Bw. Hassan Bomboko Akiongea na vijana wa kata ya Kunduchi mapema jana jijini Dar es salaam.
Vijana wa UVCCM kata ya Kunduchi wakicheza singeli katika bonanza la vijana wa kata hiyo mapema jana.

Katibu huyo alisema kuwa amesikitishwa sana kusikia vijana wanaziogopa fedha hizo zinazotokana na pato la Halmashauri, na kusababisha kupelekwa katika makundi mengine kama UWT, na kutoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Vijana wa kata hiyo kuhakikisha vijana hao wanapatiwa elimu sahii ya mikopo na matumizi yake.

Aliendelea kusema kuwa vijana ni haki yao kupata hizo asilimia nne kwa maendeleao yao inachotakiwa ni viongozi kujua idadi ya watu pamoja na vikundi vilivyosajiliwa na kutambulika kisheria ili iwe rahisi kufahamu namna kutoa mikopo hiyo na kuweza kurejesha fedha hizo ili wakopeshwe na wengine.

Alimalizia kwa kuwapongeza vijana wa kata hiyo kwa kufanya Bonanza hilo na kuweka michezo mbalimbali ikiwemo Mashindano ya kuvuta kamba, Riadha na mpira wa miguu, na kusema kuwa kata hiyo ni mfano wa kuigwa na kata nyingine zote kwa kuwa michezo inakutanisha makundi mengi zaidi ya watu.
Mjumbe wa Baraza kuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi Bw. Thobias Omega Akiwapa wosia vijana wa kata ya kunduchi.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi Bw. Thobias Omega alisema kuwa kitendo cha kuwa na kadi ya CCM pekee haitoshi bali ni kwa namna gani unaweza kukionyesha kipaji chako ndani ya chama ndio njia pekee ya kufikia mafanikio yako.

Aliendelea kusema kuwa ni vema kukitumia kipaji chako kwa kipindi hiki cha ujana wako, na kusisitiza kuwa kufanikiwa sio kusoma peke yake bali kuonyesha kipaji chako kwa uwezo wako wote, na hii itakusaidia kufikia malengo yako ya kukuwa kisiasa.
Mechi ya fainali kati ya Pameko Fc vs Ununio Fc.
Mshindi wa kwanza Pameko Fc baada ya kupewa zawadi ya Mbuzi na Mgeni Rasmi Bw. Hassan Bomboko.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: