Afisa Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Ayubu Masenza katikati akitoa elimu kwa wananchi waliotembelea banda lao kwenye eneo la Tangamano kulikokuwa kunafanyika maonyesha ya wiki ya vijana Kitaifa
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Malik Munis kushoto akiwaonyesha wananchi maeneo bomba la mafuta litapita  waliojitokeza kwenye banda lao

Afisa Maendeleo ya Jamii wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Eugene Isaya akiwaonyesha kitu wananchi waliojitokeza kwenye banda lao.
---
WAKAZI wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa ikiwemo kupokea mradi mpya wa bomba la gesi toka Tanga-Tanzania hadi nchini Uganda mradi ambao utakwenda sambamba na mradi mkubwa wa Bomba la Mafuta.

Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) Ayubu Masenza wakati alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mradi mkubwa wa bomba la Mafuta wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya vijana kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga

Alisema mbali ya uwepo wa mradi huo wa bomba la Mafuta toka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga-Tanzania Serikali ya Uganda ipo katika mchakato mkubwa wa Ujenzi wa mradi wa bomba la gesi litakaloanzia Jijini hapa hadi nchini Uganda.

Alisema Jiji hilo litakuwa miongoni mwa Majiji ambayo yanakuwa kwa kasi kutokana na uwepo wa miradi mikubwa barani Afrika ambayo inatarajiwa kutekelezwa na Serikali ya Tanzania na ile Uganda kutokana na ushirikiano mwema wa kiuchumi.

Aidha alisema ujio wa bomba la mafuta utakuwa na manufaa makubwa kwa wakazi wa Jiji hili la Tanga kutokana na Uganda kuhitaji gesi ya hapa nchini hivyo itakapokuwa ikitokea Mkoani Mtwara itafika mkoani hapa na itakwenda sambamba na bomba hilo hadi Uganda.

Masenza alisema uwepo wa gesi Jijini Tanga kutaongeza fursa za
wawekezaji kutokana na viwanda vingi kuhitaji matumizi ya gesi katika shughuli zote za uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

Alisema mbali na uwepo wa ajira kupitia miradi hiyo pia ongezeko la matumizi ya gesi litakuwa kubwa hasa katika viwanda, mashule,taasisi za kijeshi,Hospitali,na mwananchi mmoja mmoja jambo ambalo linaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.

Alisema hatua zote muhimu za utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa umekwisha anza na zipo katika hatua nzuri huku jambo la msingi kwa wananchi kuwa na utayari ili kunufaika na fursa hizo.

“Nijukumu la wananchi wa Tanga sasa kuweza kunufaika mbali na Serikali lakini mwamanchi mmojammoja wananafasi kubwa kunufaika na miradi hii itakayoweza kubadilisha maisha yao kwa ujumla.

Hata hivyo alisema mradi huo wa bomba la mafuta utapitia mikoa
nane,wilaya 24,kata 184 na Vijiji 270 huku matarajio ya maeneo hayo ni kupitia wa mradi wa bomba hilo la gesi kutokana na ujenzi wake utakwenda sambamba.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: