Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akiwa na Zumbe wa Kitulwe Tibua Charles Nkuninga kulia wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye Tamasha la Bonde ambalo lilifanyika Kata ya Kicheba wilayani Muheza lililokwenda sambamba na maonyesho ya vitu mbalimbali vya asili ikiwemo vyakula.
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akizungumza wakati wa Tamasha hilo
Afisa Utamaduni wa wilaya ya Muheza Msafiri Charles Nyaluka akizungumza katika Tamasha hilo.
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu akiingia kwenye Tamasha hilo
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kushoto akitazama bidhaa mbalimbali vinavyotengenezwa na wakima mama wa Kibondei wakati alipotembelea Maonyesho hayo wakati Tamasha la Bonde lililofanyika eneo la Kicheba wilayani Muheza.
MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu kulia akilakiwa na wananchi wa Kijiji Kicheba Kata ya Kicheba wilayani Muheza wakati alipokwenda kwenye Tamasha la Bonde.
Sehemu ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakifuatilia Tamasha hilo.
Ngoma ya Mdumangi ikiendelea kuchezwa.
Ngoma ya Mdumange ikiendelea kuchezwa.

MBUNGE wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu amewataka vijana wilayani humo kuacha kuvaa suruali na kuzishusha chini maarufu kama milegezo, mini sketi kwani kufanya hivyo kunapelekea kuondoa utamaduni wa kitanzania hususani za watu wa bonde kupotea badala yake wavae nguo za asili zenye heshima.

Kwani uvaaji huo wa nguo unapelekea kupoteza mila na tamaduni ambao uliopo huku akiwataka kubadilika kwa kuhakikisha wanavaa mavazi asili ambayo ni desturi kwa watanzania.

Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu wakati wa Tamasha la Bonde ambalo lilifanyika Kata ya Kicheba wilayani Muheza lililokwenda sambamba na maonyesho ya vitu mbalimbali vya asili ikiwemo vyakula.

“Tamasha la Bonde linapaswa tuliendeleze kwa vizazi vya sasa na vijavyo waweze kujua tamaduni na mila zao ...lakini pia mambo ya mavazi badala ya kuvaa milegezo, mini sketi huku mavazi na desturi zetu vinapotea tuvae nguo za asili zenye heshima kwani bila kufanya hivyo mavazi na desturi vitapotea”Alisema Mbunge huyo

Mbunge huyo alisema pia ni muhimu tamaduni za kibondei kuhakikisha zinaendelezwa kila mwaka kupitia tamasha hilo kwa kuyafadili ili vijazi vya sasa na vijavyo viweze kujua mila zao huku akiwasisitiza wazee waliopo kutokuondoka nazo maana vijana wanaozaliwa wanaweza kuona mambo hayo hayawezekani.

Awali akizungumza katika Tamasha hilo Zumbe wa Kitulwe Tibua Charles Nkuninga alivitaka vizazi vitumie teknolojia ya sasa kuweza kuendeleza mila kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, instragram, youtube na whatspp.

“Lakin pamoja na mambo hayo lakini tamasha hili ni hatua moja linatupeleka mbele zaidi kwa sababu kitu ambacho ni changamoto tunatakiwa tukitatue uzoefu hata lugha kwani wapo baadhi ya vijana wengi hawajui lugha yao ya asili”Alisema

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya Mstaafu Samweli Kamote alisema analifurahi tamasha hilo kwa maana malezi ya zamani waliokulia wao yanaanza kupotea yaliyokuwa yanalenga kwenye nidhamu,utii kwa vijana.

Kamote alisema hivyo kufanyika kwa tamasha kila mwaka kunafufua ari ya kufanya mila na desturi zilizokuwa na malezi na maadili kwa vijana zinarudishwa kwani sasa utandawazi umetawala dunia vijana wanaharibika.

“Labda niwaambia kwamba tukiendeleza tamasha hili kila mwaka tutasaidia kurudisha nidhamu ya maadili kila mwaka na kutokusahau kupotea kwa lugha ambazo ndio msingi muhimu “Alisema.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: