Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya NMB mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Meneja Mahusiano Wakala na Mauzo NMB Makao Makuu, Nehemiah Simba akizungumza wakati wa mafunzo kwa mawakala wa NMB mkoa wa Shinyanga.

Meneja wa Uwakala Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Tabora,Ngarami Urassa akizungumza wakati wa mafunzo kwa mawakala wa NMB mkoa wa Shinyanga.

Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.

Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.

Meneja Mahusiano Wakala na Mauzo NMB Makao Makuu, Nehemiah Simba akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na benki ya NMB.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mafunzo hayo.

Msimamizi wa Sheria,Taratibu na Kanuni benki ya NMB Kanda ya Tabora, Janeth Uiso akitoa mada jinsi ya kuzuia vitendo vya kutakatisha fedha na kuwezesha kifedha vikundi vya kigaidi.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi zawadi ya cheti na fedha taslimu 100,000/- bi Juliana Shilatu aliyetangazwa kuwa Wakala bora wa NMB mkoa wa Shinyanga.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Saha Dachi and Company shilingi 75,000 mshindi wa nafasi ya pili ya wakala bora wa NMB.


Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika.

Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika. 


Benki ya NMB imeendesha mafunzo kwa Mawakala NMB mkoa wa Shinyanga kwa ajili kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafahamu mbinu za kudhibiti fedha haramu pamoja na mbinu za kukuza biashara zao kwa kuongeza wateja.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni alikuwa Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Melusori alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwawezesha mawakala kukuza kipato chao lakini pia namna ya kudhibiti fedha chafu/haramu ‘Money laundering’.

“Lengo jingine ni kuwasilisha na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili mawakala hawa,kuwapongeza/kutambua mchango wa mawakala wanaofanya kazi vizuri na kuwaeleza kuhusu maboresho yanayofanywa na NMB”,alisema Melusori.

Hata hivyo aliwataka mawakala wa NMB kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria halali za fedha.

“Asilimia ya watanzania wanaotumia benki ipo chini ya asilimia 20 kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni hivyo shirikiane na benki kuhakikisha kuwa watanzania ambao hawajaanza kutumia huduma ya benki kwani benki ni sehemu salama zaidi”,aliongeza.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano Wakala na Mauzo NMB Makao Makuu, Nehemiah Simba alisema benki ya NMB yenye matawi 228,ATM mashine 715 ina mawakala 7000 wa NMB nchini kati yao 75 ni wa mkoa wa Shinyanga.

“Nawapongeza mawakala wa Shinyanga kwa kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa NMB,tunajivunia sana kuwa na mawakala waadilifu,tumeamua kuwafikia kwani tunajali wateja wetu kwani lengo letu ni kutoa huduma bora,salama na zenye ufanisi”,alisema.

Alisema katika mafunzo hayo,miongoni mwa mada zilizotolewa ni pamoja na huduma zinazotolewa na NMB,Mawakala wa NMB,matumizi sahihi ya mashine za kutolea huduma,namna ya kupata mikopo na mbinu za kutambua na kudhibiti watakatishaji wa fedha ‘watu wabaya’.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: