Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Fastjet Tanzania, Capt. Arif Jinnah(kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uteuzi mpya wa Mwenyekiti Mpya wa Fastjet Tanzania Lawrence Masha. Pichani wengine ni Mwenyekiti Mtendaji Mpya wa Fastjet Tanzania, Lawrence Masha na Mkuu wa Mahusiano ya Kiserikali wa Fastjet Tanzania, Eng. August Kowero.

Mwenyekiti Mtendaji Mpya wa Shirika la Ndege Fastjet Tanzania, Lawrence Masha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uteuzi wake wa kuwa mwenyekiti wa shirika hilo. Pichani kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Fastjet Tanzania, Capt. Arif Jinnah na kushoto ni Mkuu wa Mahusiano ya Kiserikali wa Fastjet Tanzania, Eng. August Kowero.
---
Kati ya mashirika ya ndege zinazokua kwa kasi zaidi, Fastjet Airlines Ltd, Tanzania, leo imethibitisha mikakati ya kumiliki shirika hilo yanaenda vizuri.

Tarehe 6 Novemba Fastjet ilimteua Ndugu Lawrence Masha kuwa Mwenyekiti Mtendaji wa kwanza wa shirika hilo. Uteuzi huu umedhibitisha nia ya kuendelea kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi kama kampuni inayomilikiwa na Watanzania pamoja na masoko ya talii za nje.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Ndugu Masha alisema, “ tumejikita zaidi kwa watanzania ambao wamefaidika kutokana na huduma zetu kwa miaka sita sasa. Tunatarajia kuongeza kuongeza safari za ndani na pia kuongeza idadi ya ndege ambazo zinakidhi mahitaji ya soko”. Tunaona fursa kufanya kazi na kushirikiana na mashirika ya ndege za ndani na nje ya nchi pamoja na Air Tanzania kutimiza mikakati ya serikati ya utalii.

Ndugu Masha ataendeleza vizuri na mikakati ya kubadilisha shirika hilo pamoja na uongozi kuhakikisha wanatoa huduma kwa watanzania.

Fastjet imetoa huduma kwa miaka sita ambapo imesafirisha zaidi ya abiria milioni 2.5 ndani ya Tanzania pekee.

Shirika hili lenye bei nafuu lina hudumia usafiri wa ndege katika miji ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, Lusaka na Zimbabwe. Na linarekodi ya kusafirisha wastani wa abiria 30,000 kwa mwezi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: