Nianze kwa kutoa masikitiko yangu nikiwa ni mdau wa burudani na mpenda maendeleo ya nchi yangu, kwa haya mambo ambayo yamefanyika ya kusitisha Tamasha la Tigo Fiesta 2018 wakati ulishatoa kibali cha kufanyia eneo husika??? yani Leaders Club, Kinondoni Jijini Dar es Salaam binafsi sijakubaliana.

Nimesikitishwa sana, hivi unawezaje kumuacha mtu akaandaa sherehe yake vizuri na ukampa kibali mwisho wa siku ukasema oh! sitaki ufanye sherehe yako ukumbi huu labda kule... Jamani jamani hebu mamlaka husika hakuna namna inawabidi mkajitathimini. Tambueni hii ni biashara kama biashara nyingine mtu ameingia gharama ya kuandaa steji nzuri, kila kitu amekifanya kwa ustadi likiwemo suala la fursa kwa wajasiliamali nao amewapa mabanda ili wafanye biashara wajiingizie kipato leo,  tu eti hapatakiwi, kwani mwanzo hamkuona hapatakiwi??

Leo ni watu wangapi ambao wanasononeka kupitia tamasha hilo, si kwa kukosa burudani ila fursa za biashara. Serikali nayo imekosa gawiwo lake la kodi (18%) ya mapato ambayo yangepatikana. Haya mambo hayatakiwi kufumbiwa macho lazima tuseme tu ili waliohusika wajihoji upya.

Binafsi nimechukizwa na hili swala na tumshtakie mwenyezi Mungu, maombi yangu yeyote ambaye ameshiriki kwa namna moja au nyingine kukwamisha shughuli mwenyezi Mungu akaonyeshe ukuu wake.

Poleni sana Clouds Media Group, Prime Time Promotions, Tigo Tanzania na wadau wengine msife moyo hizi changamoto za duniani hakuna budi kuzikabili.

Asanteni sana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: