Afisa kazi mfawidhi mkoani Arusha Willfred Mdimu akiongea na waandishi wa habari Ofisini kwake leo jijini hapa kuelezea kukamatwa kwa Mfanyabiashara na mmiliki wa makampuni matatu ya Hanspoul group Campanies ya jijini Arusha.

Na Mwandishi wetu Arusha

Mfanyabiashara maarufu jijini Arusha na mmiliki wa viwanda vya Hans Poul Kamaljit Hanspoul (58) pamoja na wafanyakazi wake watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa kwa madai ya kuajiri wafanyakazi wasio na vibali vya kazi (raia wa kigeni)na kufanya kazi kinyume cha sheria ya kuratibu ajira za wageni.

Akizungumza na vyombo vya habari Ofisini kwake Kaimu Afisa kazi Mfawidhi mkoani hapa Willfred Mdumi Amesema kuwa jana walikuwa kwenye Operesheni ya kazi walipofika kwenye kiwanda cha Hanspoul walibaini kuwepo wafanyakazi wakigeni wanaofanya kazi kinyume cha sheria kwenye viwanda vya mfanyabiashara huyo.

Aliwataja wafanyakazi hao watatu kuwa ni Shivkumar Vemula (27)raia wa nchini India Vinoth Krishanth Sathsivam (29) raia wa Sirlanka pamoja na Raiph Leopold Hruscka( 54) raia wa Ujerumani ambao wanashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini hapa na watafikishwa mahakama hapo kesho.

Mfanyabiashara huyo ambaye ni miongoni mwa wafanyabiashara waliopo kwenye kamati ya kusaidia shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba 18 za polisi zilizungua mkoani hapa mkoani hapa anadaiwa kutenda kosa hilo kinyume na sheria sura namba 1 ya mwaka 2015 kifungu cha 9 cha sheria za kuratibu ajira za wageni.

Katika Operesheni hiyo ya mkoa inayosimamiwa na Kamishna wa kazi nchini Gabriel Malata inaendelea katika maeneo mbali mbali mkoani hapa lengo ni kuhakikisha kwamba sheria za kazi hazikiukwi na wote wanafanyakazi kwa mujibu wa sheria za hapa nchini.

Wakati huo huo mmiliki wa kampuni ya Utalii Tyche&Toya Ltd Ricardo Gramono Reto natarajiwa kupandishwa kizimbani November 30 kuajiri wafanyakazi wasio na vibali kinyume cha sheria za nchi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao na kesho watapandishwa kizimbani kujibu tuhuma mbali mbali zinazowakabili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: