Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana, Bi. Easter Riwa akizungumza na wadau na vijana walioshiriki kwenye warsha ya majadiliano kuhusu changamoto za vijana iliyofanyika Novemba 2, 2018 Morena Hoteli, Jijini Dodoma.
 Mratibu wa Mradi kutoka Shirika la Pathfinder Bi. Upendo Laizer, akitoa mada kuhusu miradi ya shirika hilo yenye lengo la kutatua changamoto mbalimbali za vijana.
 Meneja Urajibishi na Utetezi wa Shirika la Pathfinder Bw. Meshack Mollel, akielezea jambo kwa washiriki wa warsha walipokutana na vijana na wadau kujadili changamoto zinazowakabili vijana
 Baadhi ya Vijana wakifuatilia mada zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa warsha hiyo walipokutana Novemba 2, 2018 Morena hoteli Jijini Dodoma.
 Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Bw. Gerald Kihwele akiwasilisha mada kuhusu vijana wanavyohusishwa kwenye masuala ya sekta ya afya nchini.
 Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Happy Mwaipopo akichangia mada wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Morena Hoteli Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana, Bi. Easter Riwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau na vijana walipokutana Novemba 2, 2018 Jijini Dodoma kujadili changamoto za vijana kwa wadau na Serikali, na kupeana mikakati ya kukabilina na kutatua chanagamoto hizo.

NA; MWANDISHI WETU

Mfumo wa takwimu za vijana utasaidia kuandaa mikakati ya kutatua changamoto zinazowakabili na kujua mwelekeo wa maendeleo yao kwa ajili ya ustawi wa nchini.

Hayo amesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Vijana Bi. Easter Riwa wakati wa ufunguzi wa warsha ya majadiliano kuhusu changamoto za vijana kwa wadau na Serikali, iliyofanyika katika Hoteli ya Morena Novemba 2, 2018 Jijini Dodoma, alisema kuwa mfumo huo wa takwimu za vijana utawezesha kuelezea utekelezaji, mikakati na mipango mbalimbali ya maendeleo yanayowagusa vijana.

“Ni vyema kuwa na mfumo wa kitakwimu zitakazopelekea kuongeza msukumo wa utekelezaji wa majukumu kwa wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, sekta binafsi na asasi za vijana kuwekeza zaidi katika vijana.” Alisema Riwa

Aliongeza kuwa ukusanyaji wa taarifa hizi ni vyema ukahusisha na asasi za vijana ili kuashiria zoezi zima la ufanyaji wa utafiti huo kwa kushirikiana na wasimamizi wa utafiti ili kupata maoni na matokeo halisi juu ya masuala yaliyokuwa ya kitafitiwa kwa kuzingatia makundi ya vijana.

“Vijana wamekuwa wakiona upatikanaji wataarifa sio kipaumbele kwao ni kwasababu mifumo ya upatikanaji na utolewaji wa taarifa vijana bado sio rafiki, hivyo wanashindwa kuona ulinganifu kati ya taarifa zinazotolewa na kwa ajili ya maslahi yao binafsi pamoja na maendeleo za jamii zao,” alisema Riwa

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema sera ya maendeleo ya vijana imekuwa ikiwafanya wawe wenye uwezo, ari ya kutosha, uwajibikaji na wanaoshiriki kikamilifu katika nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa maendeleo yaTaifa.

Aidha, alitoa rai kwa vijana ambao wapo makazini kuwa na wao wanayo nafasi ya kushiriki kwenye mijadala hiyo ili waweze kuchangia mapendekezezo waliyonayo.

Kwa upande wake, Meneja Urajibishi na Utetezi wa Shirika la Pathfinder Bw. Meshack Mollel, alisema kuwa ushirikiano huo utawezesha kuwa na uratibu mzuri utakao washirikisha vijana na asasi hizo kuweza kupambanua changamoto zinazowakabili na kutambua fursa mbalimbali za vijana zilizopo nchini.

Naye, Mratibu wa Mradi kutoka Shirika la Pathfinder Bi. Upendo Laizer, alisema kuwa majadiliano haya yataondoa utofauti kwa vijana kwa kuwawezesha wote kutambua fursa zinazotolewa kwa ajili yao wote na si kwa ajili ya kundi fulani, hivyo tunaishukuru Serikali kwa kuendelea kuhakikisha vijana wanatumika ipasavyo katika kuhakikisha Taifa linasonga mbele.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: