Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wiki hii ameendelea na ziara yake ya kutembelea Viongozi wa Taasisi mbalimbali za Serikali ikiwa ni muendelezo wa ziara zake za kujitambulisha rasmi na  kuboresha mahusiano baina ya Benki ya CRDB na taasisi hizo.

Katika mikutano tofauti iliyofanyika siku ya Jumanne, Jumatano na Alhamisi wiki hii, Nsekela alimtembelea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna Diwani Athumani na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siang’a.

Pamoja na kufanya utambulisho rasmi kwa viongozi hao, Nsekela ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay na Maofisa wengine, alitumia pia nafasi hiyo kuwaelezea viongozi hao juu mikakati yake ya kuipeleka mbele zaidi  Benki ya CRDB na kuomba ushirikiano zaidi wa kibiashara kutoka kwa viongozi hao na taasisi wanazoziongoza.

Kwa upande wao viongozi hao waandamizi, pamoja na kumpongeza Nsekela kwa uteuzi huo mkubwa, walimuahidi kumpa ushirikiano na kumhakikishia kuwa wako tayari kuendelea kuwa wadau wakubwa wa Benki ya CRDB katika mikakati yake ya kibiashara.

Viongozi hao pia walipongeza sana jitahada za Benki ya CRDB katika kusaidia juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, zenye kulenga kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kujenga Tanzania yenye uchumi wa Kati unaoshamirishwa na viwanda.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia) pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, aliyemtembelea ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha, tangu alipoteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna Diwani Athumani (kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao chake na viongozi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (Mwenyekiti), Abdulmajid Nsekela (Mkurugenzi Mtendaji) pamoja na Tully Esther Mwambapa (Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja) ambao walimtembelea kwa lengo la kumtambulisha, Mkurugenzi Mtendaji mpya wa benki hiyo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, Kamishna Diwani Athumani (wa pili kulia) akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa.
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siang’a, akizungumza jambo wakati wa kikao chake na viongozi wa Benki ya CRDB waliomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kumtambulisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Abdulmajid Nsekela (wa tatu kushoto).
 Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Siang’a, akifurahi jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia) pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, baada ya kiko chao, ofisini kwake, jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wa pili kulia) pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Moremi Marwa wakimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa, alipokuwa akifafanua jambo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: