diamondplatnumzPart 1:-

KWA WAZEE WANGU WA BARAZA LA SANAA TANZANIA (BASATA)

Kwanza kabisa niwapongeze kwa kazi nzito na nzuri Mnayoifanya....lakini pia niwape pole kwa changamoto mbalimbali mnazokutana nazo, maana najua ugumu mnaopitia katika kusimamia sanaa yetu Nchini... Ujumbe wenu kuhusu Kufungiwa wimbo wa #Mwanza almaarufu kama #NYEGEZI wakuu nimeupata ila tu kwabahati mbaya mtoto wenu niko Canada katika harakati za kutafta rizki ili kuendelea kulijenga taifa na kuendelea kutangaza sanaa zetu, ila laiti ningelikuwa nchini ningekujamara moja kama mnavyonijuaga pindi mniitapo basi hufika haraka bila ukaidi...

Tuki wama Wasani ambao tumesajiliwa tuna kila haki ya kuheshimu na kutii baraza letu la sanaa BASATA pindi linapotoa tamko... kwasababu wao ndio wazazi na walezi wetu kwenye hii sanaa... na kwakutambua kuwa Sanaa ni kazi ya Ubunifu, na kwenye kubuni wakati mwingine kuna kuwa na usawa na wakati mwingine kutokuwa sawa ndiomaana mliteuliwa Nyinyi wazee wetu maalum kwa jili ya kuhakikisha wasanii wanapotoka nje ya Mstari mnawarudisha ili tuwe na sanaa ilio bora, tuzidi kufanikiwa, na kukua vyema na hata wasanii, mashabiki pamoja na taifa kwa ujumla lijivunie na linufaike na sanaa.....

ila Kwenye UFUNGIWAJI huu nami nilikuwa nina OMBI ama PENDEKEZO kwa baraza letu pendwa la sanaa Tanzania (BASATA)...

Licha ya kuwa ni kweli #NYEGEZI ni eneo na kituo cha Mabasi kilichopo MWANZA, lakini pia ni vyema Kama baraza letu pendwa la sanaa kutambua pia kuwa sio kila Nyimbo ni kwajili ya watoto wadogo....Hivyo kusema isipigwe kwenye TV na Radio tumekubali, lakini iwe Kwenye Ule muda ambao serikali uliuweka wa kuwa watoto wako macho, ila pale wanapolala, basi uruhusiwe ili walengwa wautazame.... PILI:- kusema tuifute Mitandaoni pia, naomba pia Baraza letu pendwa litutazame pia na hapo.... kwasababu mtoto mdogo tunaemlenga kumlinda asiharibikiwe kimaadili hapa, sizani kama mzazi wake anaweza kumruhusu akaperuziperuzi bila mipaka mitandaoni maana kama kweli ana uwezo wa kufanya hivyo basi anauwezo wa kwenda kuangalia hata Video za utupu, na vitu vingine ambayo wote tunafahamu ndio hatari na Madhara zaidi kwa watoto, kuliko hichi kinyimbo chetu cha #MWANZA NYEGEZI.

diamondplatnumzPART 2:- TATU:- Wazee wetu, vijana wenu ama wasanii wenu sasahivi tumefanikiwa kuingia kwenye masoko mbalimbali hivyo sio kila nyimbo ni kwajili ya soko la nyumbani Tanzania tu, mfano: UGANDA kuna Tamasha Linaitwa NYEGE FESTIVAL....na kwa nafasi niliyonayo UGANDA na kwajinsi nyimbo hii ilivyovuma kwa kishindo kila kona ndani ya siku tatu tu Viewers 1.5+ Millions Youtube, basi naamini kabisa Mwakani lazima NYEGE FETIVAL waniite kutumbuiza...na kama mnavyofahamu bei zangu huwaga si chini dola elf Sabini za kimarekani ( $70,000) kwa show

sawa na milioni (160,300,000 za kitanzania)....mbazo kwa show moja tu ningeweza kuchangia pato la kodi si chini ya milioni (48,090,000 ya kitanzania)...hivyo naomba mlitazame na hapo Balaza letu Pendwa....

NNE:- Pia ikija Upande wa Kuitumbwiza stejini naomba pia mlitazame zaidi...Maana show zetu zote ni za Usiku wa manane ambapo watoto wamelala majumbani Tunaowaimbia ni Watu wazima...

na hata #WasafiFestival2018 pia ifikapo saa 12 jioni ni wenye Umri wa zaidi ya miaka 18 tu....hivyo tutaowaimbia ni watu wazima tu

TANO:- Wazee wangu wa Balaza la sanaa BASATA nilikuwa naomba Muipe sikio tena Nyimbo pale kwenye kipande cha Amber Rutty.. kwasababu Ujumbe wangu pale ni kupingana na kile kitendo, na ndiomaana nikasema "kananivuta ghetto nikapige Bunduki,... ila naogopa Centro Michezo ya Amber Rutty" ....sasa hapo ubaya wake uko sehem gani...maana naamini kupitia mstari huo utakuwa ni kama Kumbusho kwa kijana ama mtuyoyote kuwa "usidiriki kufanya, Utapelekwa jela..." sasa hapo wapi ubaya wake wazee wetu....

SITA:- wazee wangu wa BASATA ni siku tatu tu Tangu kutoka kwa wimbo huu, lakini kika Mwana Afrika na hata asiyekuwa Mwana Afrika Ashapajua Nyegezi Mwanza....na naamini kulikuwa na wengi pengine hawapajui lakini kupitia wimbo Huu sasa wamepajua..na naamini wengi wanatamani hata wafike, Wapigepicha , wakapashangae kuwa kumbe #NYEGEZI kwenyewe ndio hapa....na hiyo ndiuo miongoni mwa faida ya kazi ya sanaa wazee wetu....

Mie yangu yalikuwa ni hayo tu, naamini Kwa Uelewa wenu na Upendo wenu mlionao kwa sanaa na wasanii wenu, mtatusaidia kwa hayo maombi yetu vijana wenu...Shukran

Ni mimi kijana wenu

Nasibu Abdul Juma
(Diamond Platnumz)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: