Habari Tanzania. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru sana Watanzani wote na wasio Watanzani kwa maombi yeni juu ya mashindano ya New York City Marathon ingawa mimi nimeshindwa kufanya vizuri na pia nimeshindwa kumaliza kabisa.

Naomba niwatie moyo tusikate tamaa kwani bado kuna mashindano mengi mbele tuendee kumwomba mungu ili atusaidie wachezaji wa Kitanzania tuendee kuiwakilisha nchi yetu vyema katika mashindano mbali mbali yajayo.

Tukumbuke kuwa kila jambo linachangamoto zake.

Na napenda kuwaambia sio kila mara itakuwa wewe kuna wakati wa kupanda na wa kushuka pia kwenye mafanikio tufurahi na kwenye shida tushikamane.

Nawashukuru sana na Mungu awabariki. Amen.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: