Viongozi wapewa maagizo mazito

Na Mwandishi wetu, Mihambwe

Viongozi wa Vijiji na Vitongoji wametakiwa kutumia madaraka yao vyema kwa kutokuwa chanzo cha migogoro ya ardhi na mipaka katika jamii wanazo ziongoza.

Hayo yamesemwa na Afisa Tarafa Mihambwe, Gavana Emmanuel Shilatu alipokuwa akizungumza na viongozi wa Serikali za Vijiji vya Mwenge A na Namunda vilivyopo kata ya Kitama ambao kwa muda mrefu wamekuwa kwenye mgogoro baridi wa kugombea kipande cha ardhi cha mpaka.

Katika kikao hicho cha awali kuelekea kupata ufumbuzi wa kudumu Gavana Shilatu aliwapa maagizo mazito ya kuzingatiwa na pande zote za Serikali za vijiji.

*"Ni aibu kwa Viongozi kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi na mipaka, huku ni kutumia vibaya madaraka yenu. Kuanzia sasa natoa maagizo kwenye kile kipande kidogo cha mpaka wa ardhi chenye utata ni marufuku kwa pande zote kuuza ardhi ama kuamua kujiwekea mipaka kienyeji enyeji mpaka pale timu ya Maafisa ardhi watakapokuja kubainisha mipaka halisia.*" alisema Gavana Shilatu

Maagizo aliyotoa Gavana Shilatu yaliungwa mkono na pande zote za Serikali za Vijiji walioahidi kuyatekeleza na kutoa ushirikiano wakati wowote watakapo hitajika.

*"Naomba tuendelee kushirikiana, kushikamana, tuishi kwa amani na upendo kama awali hakuna kitakacho haribika."* alimalizia Gavana Shilatu.

Katika kikao hicho kilihudhuliwa na Diwani kata ya Kitama, Mtendaji kata ya Kitama, Afisa Maendeleo kata ya Kitama, Wazee maarufu, viongozi wastaafu wa Serikali zilizopita pamoja na viongozi wa Serikali za sasa za Vijiji vya Mwenge A na Namunda kilimalizika kwa amani, utulivu na furaha kwa pande zote.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: