Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini Dkt. Abdallah Saqware Baghayo akizungumza na waalimu, viongozi wa kijiji cha Gedamar 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Bima ya Jubilee. Dipankar Acharya
Meneja wa TIRA Kanda ya Kaskazini Eliezer Rweikiza
Mkuu wa Kitengo cha fedha kutoka Jubilee Life Insuarence Helena Mzena akizungumza katika hafla hiyo
Meneja wa Kampuni ya Bima Jubilee Kanda ya Kaskazini Sweetbert Lasway akizungunza na wazazi na wanafunzi katika shule ya msingi Gedamar
Kamishana wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Nchini Dkt.Abdallah Saqware akibadilishana mawazo na viongozi wa kijiji cha Gendemar pamoja na waalimu wa shule ya msingi Gendermar
Picha ya pamoja. Picha zote na Vero Ignatus

Vero Ignatus, Manyara. 

Kamishna wa Bima Tanzania Dkt.Abdallah Saqware Baghayo amewata wafanyabiashara hapa nchini wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi kwa kutumia njia ya magari,ndege,meli ikatiwe Bima kutoka katika makampuni yaliyosajiliwa na mamlaka hiyo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Madarasa Mawili Ofisi Pamoja na Vyoo katika shule ya msingi Gedamar iliyopo Wilayani Babati Mkoani Manyara,Baghayo amesema ni kosa kwa mfanyabiashara kisheria kwa mfanyabiashara kunua bidhaa ambayo haijasajiliwa na mamlaka hiyo.

Amesema ni tegemeo la serikali kuwa makampuni yaliyopewa leseni yatapata biashara ya uagizaji wa bidhaa huku akiwataka wananchi kutambua umuhimu wa bima na kufuata sheria.

Dkt.Baghayo amesema mabadiliko ya sheria hiyo yalisainiwa na raisi Dkt.John Pombe Magufuli ili kuweza kutekelezwa na kuzuia wafanyabiashara kutumia bima kupitia makampuni yasiyo sajiliwa.

Kwa Upande wake Mkuu wa Kitengo cha fedha kutoka Jubilee Life Insuarence Helena Mzena alisema kuwa kampuni hiyo inatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake, hivyo kuamua kurudisha faida kwa jamii kwa kuangalia changamoto mbali mbali zilizopo katika shule ya msingi hapa nchini.

Aidha alisema kuwa mradi huo walipanga kutumia kiasi cha shilingi Milioni 200 kwa Ajili ya kukarabati Vyumba vya Madarasa,Ujenzi wa Vyoo,Ujenzi wa Nyumba mbili za walimu na Ujenzi wa Ofisi ya Walimu kulingana na mahitaji ya shule husika.

Mzena alisema kuwa Kampuni hiyo mpaka sasa imetumia kiasi cha shilingi milioni 152 katika Shule saba katika Mikoa ya Morogoro,Manyara,Bukoba,Mbeya,Dar es Saalam,Dodoma na Zanzibar.

Naye Meneja wa Kanda ya Kaskazini Sweetbert Lasway alisema kuwa kampuni hiyo imeweza kukarabati madarasa mawili,Kumalizia Ofisi ya walimu na Ujenzi wa Vyoo katika shule ya msingi Gedamar kwa gharama ya shilingi milioni 25.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: