Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Muigizaji maarufu wa Filamu Tanzania, Wema Sepetu (kulia) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba Mosi, 2018 majira ya subuhi akikabiliwa na shtaka moja la kuchapisha picha za ngono mtandaoni.

Wema ambaye pia ni miss Tanzania mwaka 2006, anashtakiwa chini ya kifungu cha sheria namba 14(1)(b) na( 2) (b) cha makosa ya mtandao

Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amedai mbele ya Hakimu Mkazi Maira Kasonde kuwa Oktoba 15.2018, katika maeneo tofauti tofauti jijini, mshtakiwa Wema kupitia ukurasa wake wa Instagram, alichapisha Picha za ya video za ngono (Phonograph).

Hata hivyo, Wemma ambaye alitinga kizimbani majira ya saa saba kasorobo mchana amekana kutenda kosa hilo.

Wakili anayemtetea Wema, Simwanza Rubeni ameiomba mahakama kumpatia mteja wake dhamana kwa kuwa shtaka linalomkabili mshtakiwa Wema linadhaminika kisamesema Pia ameiomba mahakama kumpatia mteja wake huyo masharti nafuu ya dhamana.

Hata wakili Kombakono alipinga na kuiomba mahakama kumpatia mshtakiwa huyo masharti magumu ya dhamana kwani kitendo alichofanya kijamii na kimaadili linapingana kabisa na maadili ya Tanzania,
Amedai mshtakiwa Wema pia anafollowers wengi sana kwenye ukurasa wake wakiwemo watoto wadogo ambao wanakuwa wanafuatilia kile anachofanya.

"Tunaomba mahakama ikiwezekana iweke masharti magumu kwake ili iwe fundisho kwa wale ambao wangependa kuiga kile ambacho amesema Kombakono..

Wakili Simwanza amepinga hoja hizo na kudai dhamana ni haki kikamesema wakilihivyo kiweka masharti magumu kwake ni kama vile umeishamuhukumu" amesema wakili Simwanza

hilo na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana.
Mahakama imemtaka Wema mwenyewe kisaini bondi ya sh. Milioni 10 na kuwa na mdhamini mmoja ambaye atakayesaini bondi ya kiasi hicho cha fedha.

Pia Mahakama imempiga marufuku mshtakiwa Wema kutochapisha Picha yoyote ya ngono katika ukurasa wake wa Instagram au kuchapisha maneno yoyote yenye viashiria vya ngono.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 20, 2018 Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: