Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu (kulia) akisikiliza maelezo ya namna Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini inavyotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo vijijini yenye lengo la kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ikiwemo mazingira, wakati wa Mahafali ya 32 yaliyofanyika katika Kampasi ya Dodoma.

Mlau wa Mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Dkt. Christina Mandala, akiongoza maandamano wakati wa mahafali ya 32 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Dodoma, ambapo wahitimu 2596 wametunukiwa vyeti na shahada mbalimbali. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho Prof. Hozen Mayaya na kushoto ni Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi chuoni hapo Bi. Mugabe Mtani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatib Kazungu akihutubia wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo hicho, Dodoma.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini, Prof. Hozen Mayaya, akitoa taarifa ya maendeleo ya Chuo kwa wahitimu na wageni mbalimbali waliohudhuria katika mahafali ya 32 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika Kampasi ya Chuo, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akimtunuku Shahada ya Uzamili, mmoja wa wahitimu katika mahafali ya 32 ya chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini yaliyofanyika katika Kampasi ya chuo hicho, Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini akitunuku wahitimu wa kada mbalimbali katika mahafali hayo kampasi ya Dodoma.
Wahadhili wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Prof. Youze Mnguu (kushoto) na Prof. Zacharia Masanyiwa, wakifuatilia kwa makini matukio wakati wa Mahafali ya 32 ya Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini akitunuku wahitimu wa kada mbalimbali katika mahafali hayo Kampasi ya Dodoma
Baadhi ya wahitimu wa kada mbalimbali katika chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini wakiwa katika sherehe za mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo cha Maendeleo Vijijini wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu, wakati wa Mahafali ya 32 yaliyofanyika chuoni hapo Jijini Dodoma.  (Picha na Saidina Msangi-Wizara ya Fedha na Mipango)


Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: