Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na Vyombo vya Habari leo Jijini Dar es Salaam, akifafanua mstakabadhi juu ya suala la uchaguzi mkuu wa Yanga, ambapo Serikali iliingilia kati suala hilo kwa kushirikiana na Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF, Baraza la michezo Tanzania BMT pamoja na uongozi wa Klabu ya Yanga, na kuamua ufanyike tarehe hiyo hiyo ilivyopangwa hapo awali, Januari 13 mwakani.

Na Agness Francis, Blogu ya Jamii.

SERIKALI imesisitiza mustakabali wa tarehe ya uchaguzi mkuu wa Klabu ya Yanga kufanyika Januari 13 mwakani kama ilivyopangwa hapo awali.

Amesema hayo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe leo katika ukumbi wa uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam baada ya kukubaliana kwa pande zote, shirikisho la Mpira wa miguuTanzania (TFF), Baraza la michezo Tanzania BMT pamoja na uongozi wa Klabu ya Yanga.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa wamehimiza kamati ya uchanguzi ya Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF ishiriki kwa karibu sana na kamati ya uchanguzi ya Klabu ya Yanga waliochaguliwa kusimamia uchaguzi huo ili kuokoa soka la Tanzania kusonga mbele.

Aidha Dkt Mwakyembe amesema kamaa wizara hawaitambui hoja ya wanachama wa Yanga suala la kuwa aliekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kuwa bado anakaimu nafasi hiyo Klabuni hapo.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa kama alikuwa anajua yeye bado ni Mwenyekiti wa Yanga angepaswa kuhudhuria vikao, lakini takribani kama vikao 10 vya wajumbe hakuhudhuria ambapo pia hajafanya kazi katika Klabu hiyo ndani ya mwaka.

"Na sisi tumesema Kama wanachama wana mtaka aendele kuwa kiongozi wa Klabu ya Yanga wamchukuliwe fomu ya uchaguzi lakini cha kushangaza mpaka sasa hajachukuliwa, kurudi kwake Manji ni lazima achukue fomu" amesema waziri Mwakyembe.

Dkt Mwakyembe amesisizia kuwa wanachama wa Yanga wajitokeze kwa wingi kupiga kura ili kuifanya timu yao kuwa imara na kuepukana na migogoro ya kila siku isiyoleta faida kwao.

"Yanga ni Klabu kubwa hapa nchini ikiteseka soka la Tanzania litateseka kwa ujumla, wanachama wajitokeze kupiga kura kuchagua kiongozi atakayekuwa ana maslahi na manufaa kwa timu yao" amesema Mwakyembe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: