Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akizungumza na waaandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa wilaya ya Kigamboni,Sara Msafiri akimkabidhi kitambulisho cha mjasiriamali,Amina Rashidi jana jijini Dar es Slaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoa wa Temeke,Gamaliel Mafie akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Wilaya ya Kigamboni imeongoza katika utoaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali katika mpango wa kuwatambua wafanyabiashara wadogo wadogo baada ya kuwa ya kwanza katika Mkoa wa Dar es salaam kuwafikia wafanybiashara wengi zaidi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Sara Msafiri alipokutana na wandishi wa habari ofisini kwake jana. Mkuu wa Wilaya amesema ofisi yake ilipokea vitambulisho elfu tano toka ofisi ya Rais-Tamisemi na vikiwa na lengo la kukusanya jumla ya shilingi Milioni mia moja lakini mpaka jana Desemba 28,2018 jumla ya shilingi milioni 94 sawa na asilimia 97 ya lengo.

Mkuu wa Wilaya amesema kuwa kiwango hicho kimefikiwa baada ya kuwa na mpango wa ushirikishwaji wa watendaji wa mitaa na wenyeviti ambapo waliweza kuwafikia wajasiriamali wengi katika mitaa yao.

Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato (TRA) Mkoa wa Temeke Bw.Gamaliel Mafie amesema wao kama mamlaka wamefurahia huo mpango kwa kuwa umewajumuisha watu ambao hawakuwa kwenye mfumo rasmi wa walipa kodi. Ameongeza kuwa hata wao wamepokea mpango huo kwa furaha kwa kuwa umepanua wigo wa walipa kodi kwa mpango wa kuchangia.

Akihitimisha kikao hicho, Mkuu wa Wilaya ametuma ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili aweze kupatiwa vitambulisho elfu tatu (3000), kukidhi idadi kubwa ya wafanyabishara ambao bado hawajafikiwa mpaka sasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: