Rais Dkt. Magufuli: Nia aibu kwa Taifa lenye watu milioni 55 kuwa na walipa kodi milioni 2.2 pekee. Kenya ina watu milioni 46 na walipa kodi milioni 3.9

Rais Dk. John Pombe Magufuli, akiwa katika Kikao Maalum kati yake na Uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ameeleza kuwa, Tanzania haifanyi vizuri katika suala la ukusanyaji wa mapato kulinganisha na Nchi nyingine za kiafrika.

Alieleza kwa kufafanua takwimu za kodi kwa kulinganisha Tanzania dhidi ya majirani zake:

1. Tanzania (milioni 55): walipa kodi milioni 2.2; kodi inayotozwa ni 12% ya GDP.

2. Kenya (milioni 46): walipa kodi milioni 3.9; kodi inayotozwa ni 18% ya GDP.

3. Uganda (milioni 37): walipa kodi milioni 1.2; kodi inayotozwa ni 14% ya GDP.

4. South Africa (milioni 56): walipa kodi milioni 19.9; kodi ni 26% ya GDP.

5. Mozambique (milioni 5.3): walipa kodi milioni 5.3; kodi ni 18% ya GDP.

6. Zambia (milioni 16): walipa kodi milioni ?; kodi ni 15% ya GDP.

7. Botswana (milioni 2): walipa kodi milioni 0.7; kodi 14% ya GDP.

8. Burundi (milioni 10): walipa kodi milioni 0.2; kodi 13% ya GDP.

9. Namibia (milioni 2): walipa kodi milioni 0.6; kodi 12% ya GDP.

Hapa Rais Magufuli amepigilia msumari kwenye ukweli.

Watanzania wamekuwa wakilalamika kuwa, kodi ni nyingi na kwamba Sera za sasa siyo rafiki kwa mazingira ya kibiashara na uwekezaji nchini. Sasa ukweli umewekwa wazi kuwa, Tanzania ndiyo Nchi yenye wastani mdogo sana wa walipa kodi katika Nchi zote za Afrika Mashariki.

Vilevile, mapato yatokanayo na kodi nchini Tanzania, ni asilimia ndogo sana kulinganisha na Nchi majirani. Tanzania imepigwa na Kenya, Uganda, Zambia, Msumbiji, Rwanda, Burundi, SA, Botswana na Namibia katika asilimia ya Mapato yatokanayo na kodi (kiwango cha kodi kulinganisha na uwiano wa pato la Taifa).

Sasa wewe fikiria, kama Serikali ya sasa imejitahidi kuziba mianya ya kodi na kuongeza walipa kodi lakini bado Tanzania iko nyuma kulinganisha na majirani zake, je kipindi cha kabla ya Magufuli, hali nchini ilikuwaje?

Tatizo liko kwa Watanzania wenyewe. Sera za ovyo za kuwarahisishia maisha watu wavivu ndizo zilizotufikisha hapa. Tuliifanya Tanzania masikini kuwa Nchi inayotegemea consumer goods na kujisahaulisha misingi ya kiuchumi.

Leo bado tuko nyuma kwenye kodi but tunalialia, sasa hali ikifika ya kuifanya kodi kuchangia asilimia 15% itakuwaje.

Tuaje uvivu, majirani walikuwa wanatuchora sana kipindi cha nyuma namna tulivyokuwa tunapotea. Sasa hivi tunaifanya Tanzania kuwa Nchi ya kuzalisha bidhaa zetu na siyo kupokea kila kitu kutoka nje.

Rais Magufuli amewakumbusha Watanzania kuwa: Hapa duniani, mambo ya uhakika ni mawili pekee: kifo na kukusanya kodi.

Kuna watu walikuwa kutwa wanashauri haya mambo yafanyike . Sasa Rais Magufuli amefanya kweli. Wasipounga mkono jitihada hizi walizoshauri tutajua mabepari uchwara wamewapa posho.

Yaliyojiri kikao cha Rais Magufuli na Mawaziri, Makatibu Wakuu, MaRCs, MaRAS na TRA -
Tarehe 10/12/2018
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: