Na MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

MTOTO Manahil Mundhir Rashid mwenye umri wa miaka mitano (pichani), amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha eneo la Mkunazini mjini Unguja Visiwani Zanzibar.

Baba wa mtoto Mundhir Rashid, amesema kuwa mtoto wake alipotea Oktoba 14, mwaka huu baada ya kushuka kwenye basi wakati akitoka shule.

“Nipo kwenye mashaka ni zaidi ya miezi miwili sasa sijamuona mtoto wangu sijui yuko wapi na kwenye mazingira gani Mungu wangu.

“Binafsi nina mashaka makubwa na usalama wa mtoto wangu na hata mimi na mke wangu. Tumejawa na hofu ni wapi alipo mtoto wetu,” amesema Rashid.

Kutokana na hali hiyo amesema walitoa taarifa Kituo cha Polisi Madema mjini Unguja ambapo lilifunguliwa jalada ya uchunguzi namba MAD/R.B 8011/18.

Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya polisi ilieleza kuwa tayari mtu mmoja ameshakamatwa Oktoba 17, mwaka huu katika Bandari ya Malindi, Zanzibar kwa kosa hilo la kudaiwa kutorosha mtoto.

Baba huyo wa mtoto huyo aliwaomba wananchi kwa yeyote atakayemuona atoe kituo kituo chochote cha polisi kilicho karibu yake au awasiliane na baba mzazi wa mtoto huyo kwa namba ya simu 0773044899
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: