Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL, David Tarimo ( kushoto) akimuonyesha gari aina ya Renauld Kwid mshindi wa pili wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. Frank Nathan na mkewe ,Tumaini Patric,muda mfupi baada ya kumkabidhi gari katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya Wateja wa TBL,David Tarimo ( wapili kushoto) akimkabidhi kadi ya gari mshindi wa pili wa droo ya promosheni ya TBL Kumenoga,Frank Nathan mkazi wa Iringa wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam,wengine katika picha kutoka kulia ni Meneja chapa wa Konyagi na Wine Isaria Kilewo na Meneja masuala endelevu wa TBL Irene Mutiganzi na (wa kwanza kushoto) ni Tumaini Patric ,mke wa mshindi
Mshindi wa gari Frank Nathan na mkewe Tumaini Patric ndani ya gari lao.
Mshindi wa gari ,Frank Nathan na mke wake Tumaini Patric katika picha ya pamoja na maofisa wa TBL baada ya kukabidhiwa gari
---
Mkazi wa Iringa, Bw. Frank Nathan (38), ambaye wiki iliyopita alijishindia gari kupitia droo ya pili ya promosheni ya wateja ya kampuni ya TBL ijulikanayo kama ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ amekabidhiwa rasmi gari alilojishindia aina ya Renault KWID katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Akiongea kwa furaha baada ya kukabidhiwa gari alisema kuwa tangu apatiwe taarifa za kushinda, alikuwa anajiona kama anaota ila baada ya kukabidhiwa gari lake ndio ameamini kuwa amepata bahati ya kushinda zawadi kubwa ya gari mpya.

“Nilipopigiwa simu nakufahamishwa kuwa nimeshinda sikuamini hadi niliposoma habari juu ya ushindi wangu kwenye vyombo vya habari na baadaye kupigiwa simu kutoka TBL, Ninayo furaha kubwa kwa ushindi huu, nitasherekea sikukuu ijayo ya Krismas na mwaka mpya nikiwa namiliki gari mpya, namshukuru Mungu ameniona kupitia promosheni hii”, alisema Nathan kwa furaha.

Meneja wa Udhamini na Mawasiliano ya wateja wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL alimpongeza mshindi huyo baada ya kumkabidhi gari na kutoa wito kwa wateja wote wa vinywaji vya TBL nchini, kuendelea kuichangamkia promosheni hii ili kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi kubwa ya gari mpya aina ya Renault KWID.

“Tunayo furaha kubwa kumkabidhi zawadi yake mshindi wetu wa pili wa mwezi ambayo ni gari mpya, kwa sasa imebaki gari moja na zawadi nyinginezo nyingi kwa ajili ya wateja wetu watakaoshiriki promosheni hii hususani katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye msimu za sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya” alisema Tarimo. Tarimo, na kuongeza kuwa, promosheni hii inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa wiki yaani Ijumaa, Jumamosi na Jumapili kupitia bia za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager.

Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, alisema promosheni inafanyika kwenye mabaa zaidi ya 5,000 nchini kote. “Wateja wetu wazidi kuitafuta bendera ya TBL Kumenoga, kwani ilipo bendera hii ndipo wateja na TBL wanapokutana katika promosheni.

Alifafanua zaidi kuwa ili kuingia kwenye droo ya kujishindia gari jipya kupitia promosheni hii ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ mteja atatakiwa kununua bia tatu kati ya Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite au Balimi Extra Lager kwenye promosheni, ambapo atapatiwa kuponi yenye namba, kisha anatakiwa kutuma namba hiyo kwa meseji kwenda 15451, hii ni kwa wateja wenye mitandao ya VODACOM, TIGO na AIRTEL. Kwa wateja wa mitandao mingine watatuma namba iliyo kwenye kuponi kupitia tovuti ya www.tblkumenoga.co.tz.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: