Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Bw. Apson Mwang’onda Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, alipomtembela Ikulu jijini Dar es Salaam.Disemba 6,2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaMheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Bw. Apson Mwang’onda Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, wakati wanaagana mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.Disemba 6,2018.
---
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Desemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. Apson Mwang’onda, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Bw. Apson Mwang’onda amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kukubali ombi lake la kumuona na kuzungumza naye na amempongeza kwa uongozi mzuri unaochochea kasi ya maendeleo hususani katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

Bw. Apson Mwang’onda ameitaja baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo kuwa ni mradi wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji (Stieglers’ Gorge Power Project) na Ujenzi wa madaraja na barabara ambazo licha ya kurahisisha usafiri zitasaidia kuondoa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

“Mabadiliko ni makubwa sana ambayo yametokea, kuna miradi mikubwa mingi inafanyika sasa hivi, kwa hiyo mabadiliko ni makubwa kusema kweli na yote hayo ni kwa manufaa ya nchi, kwa hiyo nachoweza kusema amefanya kazi kubwa kwa maendeleo ya nchi” amesema Bw. Apson Mwang’onda.

Ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu ya Tano ili itekeleze mipango yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya Taifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: