Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) akizungumza na wanahabari wakati akitangaza ushirikiano wa Kampuni ya Tigo na Uber katika kuwawezesha wateja kutumia usafiri wa Helikopta.
Meneja wa Uber nchini Tanzania, Bw Alfred Msemo akizungumza na wanahabari kufafanua jinsi walivyojipanga kuwawezesha wateja wa Uber na Tigo kupata usafiri wa UberCHOPPER. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari (kushoto) akipeana mkono wa kufanya kazi pamoja na Meneja wa Uber nchini Tanzania, Bw Alfred Msemo (kulia).
Picha ya Pamoja.

Kampuni ya Uber kwa kushirikiana na Tigo , wametangaza kwamba itawazawadi baadhi ya wateja wake na fursa adimu ya kutalii mandhari ya jiji la Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa helikopta kwa kubonyeza simu zao siku ya Ijumaa ya tarehe 14 Disemba 2018.

Wateja 10 wa Uber na wateja wengine 10 wa Tigo watapata nafasi adimu na ya kipekee ya kutalii na kufurahia mandhari ya jiji kwa muda wa dakika 15 kupitia huduma ya uberCHOPPER. Kama wewe ni mteja wa Uber na ungependa kushiriki katika ofa hii, hakikisha unafungua app yako ya Uber siku ya Ijumaa tarehe 14 Disemba 2018 kati ya saa 3:00 Asubuhi na saa 5:00 Asubuhi na uite ndege kwenye usafiri wa uberCHOPPER unaopatikana ndani ya app.

Wateja wa Tigo kwa upande mwingine, wanatakiwa waendelee kutumia huduma za mtandao wa Tigo katika kipindi hiki chote na watajishindia zawadi nyingi kupitia promosheni ya Jigiftishe, pia watapata fursa ya kusherehekea ushindi wao kupitia safari za uberCHOPPER. Kampuni ya Tigo pia inawapa wateja wote wapya ofa ya safari za Uber bure jijini Dar es Salaam zenye thamani ya TZS 4,000.

Meneja wa Uber nchini Tanzania, Bw Alfred Msemo amesema, "Tunafuraha kubwa kutangaza ubia huu na kampuni ya Tigo na sifa kubwa inayotutambulisha na tunajivunia kama kampuni, ni kwamba tunatoa huduma ya kipekee kwa namna ambayo wateja wataifurahia kupitia huduma ya uberCHOPPER - ambayo itakuwa rahisi kama unavyoita magari ya Uber. Nitumie fursa hii kutoa mwito kwamba sote tupakue app ya Uber, tushiriki katika promosheni hii na kufurahia fursa hii adimu katika maisha yetu."

"Kama kampuni kubwa ya mtandao wa simu nchini Tanzania, kampuni ya Tigo imedhamiria kuleta njia mpya ambazo wateja wake wanaweza kutumia kuwasiliana na ulimwenguni wa nje kwa ufanisi mkubwa. Tayari wateja wa Tigo wanaweza kutumia app ya Uber bure, hawahitaji kuwa na bando kwenye simu zao, sambamba na kupata kuponi zinazowawezesha kufanya safari bila malipo yoyote. Sasa tunawapa fursa ya kusherehekea msimu wa huu kupitia safari za uberCHOPPER bure," Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari aliongeza.

Watakaoshinda watachukuliwa kutoka mahali watakapokuwa na kupelekwa eneo la Sea Cliff Resort ambako safari zote za uberCHPPER zitaanzia. Uhitaji wa huduma hii ya kipekee utakuwa mkubwa na nafasi ni chache, kwa hiyo, wahi uchangamkie fursa hii ili upate nafasi ya kufurahia huduma hii isiyokuwa na mfano wake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: