Mwanablog Khalfan Said kutoka K-vis blog akitoa mada kuhusu habari za mitandao katika Uchumi na fedha kwenye semina ya masuala ya fedha na uchumi inayofanyika kwenye tawi la Benki Kuu ya Tanzania BOT jijini Dodoma .
Khalfan Said kutoka K-vis blog akifafanua masuala mbalimbali kuhusu mitandao ya kijamii na habari za uchumi na fedha atika semina hiyo.

NINI MAANA YA MITANDAO WA KIJAMII (SOCIAL MEDIA):

Mitandao wa kijamii ni aina ya tovuti au Application inayowaruhusu watumiaji kuwasiliana kwa kuchapisha jumbe (Messages) kwa njia ya maandishi, picha au video kwa kutumia computer au Smart phones. Na tunapozungumzia mitandao ya kijamii inayofahamika sana na jamii yetu ni pamoja na Blogs, Youtube, Facebook, Instagram, Flicker, Tweeter, Whatsaap na LinkedIn

FAIDA YA MITANDAO WA KIJAMII

Mitandao ya kijamii inasaidia kutengeneza mahusiano mapya kati ya mtu na mtu, mtu na taasisi au taasisi na taasisi. Awali mitandao ya kijamii haikutiliwa maanani sana na ilichukuliwa kama majukwaa ya kupashana “umbea” tu, mfano nani kavaa nini, katembelea wapi, yuko na nani nk. Lakini kutokana na nguvu yake ya kufikia hadhira kwa haraka na kwa upana zaidi, (walaji) yaani hadhira ikaona iitumie pia katika kuhabarishana taarifa muhimu.

Kwa mantiki hiyo mitandao ya kijamii imefungua mlango mpya kabisa wa chombo kingine cha habari chenye ushawishi na uwezo mkubwa wa kutawanya habari katika kipindi kifupi tangu tukio litokee na wakati mwingine (live). Na Serikali nayo kwa kutambua “nguvu” hiyo ya kufikia hadhira kubwa na kwa haraka imeweka sheria sasa, kwa mtandao wa kijamii unaobeba maudhui ya habari lazima usajiliwe na Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano Tanzania (TCRA) kama chombo rasmi cha kupashana habari.

Baada ya utangulizi huo, sasa nijielekeze kwenye lengo mahsusi, yaani Social Media inaionaje BoT katika utoaji wake wa taarifa.

Ifahamike kwamba, taasisi Fulani inaweza ikawa haina bureaucracy katika utoaji wake wa taarifa, (That is well and good) lakini ikawa na udhaifu mkubwa wa usahihi (accuracy) wa taarifa hizo katika kuandaa na kutawanya taarifa.

Kwa jicho la Social Media, tunaionaje BoT katika eneo hili, bila kupepesa macho, na mwenzangu atanisaidia kwa hakika taarifa inayotoka BoT kwa matumizi ya habari, huwa imenyooka na haina makosa “uzembe”, sasa hili ni jambo jema sana kwa taasisi hii nyeti ya Serikali, kutoa taarifa ambazo zinakuwa “timamu”. Lakini pia, BoT inajitahidi kwa kiasi kikubwa kutumia uwepo wa Social Media kuwafikia walengwa (wadau wake). Mfano ni wa hivi majuzi tu, wakati kitengo cha Habari cha BoT kilipotoa taarifa ya Gavana kufanya mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha Saa 8 mchana, kama sikosei taarifa hiyo ya kuwaarifu waandishi ilitoka saa 5 asubuhi.

Sasa licha ya kutoka muda mfupi kabla ya tukio, waandishi walifika kwenye mkutano huo na kufanya coverage. Hii ndiyo nguvu ya Social Media.

USHAURI

Bado BoT mnaweza kuboresha zaidi quantity ya taarifa zenu, kwa kufanya video recording, na voice recording na kisha kuzituma kwenye media ili hatimaye taarifa hizi zipenye kwenye media channel zote, Mtu akitaka kuona taarifa kwa video, anaona, akitaka kusikiliza sauti anasikiliza, akitaka kuona taarifa ya maandishi na picha ya mtoa taarifa anaona.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: