Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi ambao ndio waandaaji wa Mbio za Morogoro Marathon akizungumza na wanahabari kuhusu tukio hilo litakalo fanyika kesho katika uwanja wa Jamhuri ,kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga,Kaimu Afisa Michezo mkoa wa Morogoro ,Grace Njau na kulia ni Fuhad Hussein , Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro ambao ndio wadhamini.
Medali zilizoandaliwa kwa ajili ya washiriki wa mbio hizo ambazo zitatolewa Mbili kwa kila mshiriki.
Meneja wa DSTV mkoa wa Morogoro ,Fuhad Hussein akizungumza juu ya zawadi za Ving'amuzi zitakazo tolewa kwa washindi wa mbio za Km 21 na Km 5.
Mkurugenzi wa Mbio,Robert Kaliyahe akitoa ufafanuzi wa njia zitakazo tumiwa na wakimbiaji siku ya Kesho.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii .

WAANDAAJI wa Mashindano ya Mbio za Morogoro Marathon 2018 wametangaza kutoa zawadi ya Medali mbili kwa kila mshiriki wa tukio hilo ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa tukio kubwa la kimichezo katika mkoa wa Morogoro.

Waandaaji hao ambao ni taasisi ya Itetet Sports Agency imetangaza zawadi hiyo jana mbele ya waandishi wa habari wakati wa kuzungumzia maandalizi ya Mbio hizo zitakazofanyika kesho alfajiri katika uwanja wa Jamhuri mjini humo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Itete Sports Agency ,Antipas Mgungusi alisema mbali na zawadi hizo kwa washiriki pia zipi zawadi kwa washindi wa mbio za Kilometa 21 kwa upande wa wanaume na wanawake ambapo mshindi wa kwanza atapata pesa taslimu kiasi cha sh 400,000 .

“Tuna mbio za Kilometa 21 pamoja na kilometa tano,lakini uwanjani kutakuwa na mbio za kushirikisha watoto kwa maana ya mita 100 na mita 200 ,kwa kilometa 21 mbali na pesa taslimu mshindi pia atapata king’amuzi cha DSTV kutoka kwa wadhamini kampuni ya Multchoice “alisema Mgungusi.

Alisema Mshindi wa pili atapata kiasi cha sh 250,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV,mshindi wa tatu akiambulia kitita cha Sh 150,000 pamoja na king’amuzi cha DSTV huku wale watakaoshiriki mbio za Km tano mshindi wa kwanza atapata sh 100,000 pamoja na King’amuzi cha DSTV kwa jinsia zote mbili.

“Mshindi wa pili kwa kilometa 5 tutatoa kiasi cha sh 50,000 pamoja na T shirt ,mshindi wa tatu atapata cheti pamoja na t-shirt na hii ni kwa wanawake na wanaume watakao shiriki lakini zawadi kubwa zaidi itakuwa ni udhamini kwa washindi watatu wa kilometa 21 na tani kwa wanaume watapata udhamini wa kushiriki mashindano yajayo hapo mwakani” alisema Mgungusi.

Alisema katika eneo hilo washindi hao watagharamiwa ,fedha za safari,malazi na usajili kwa ajili ya kushiriki mashindano yajayo huku wengine washiriki wengine watakaoingia hatua ya 10 bora wao watashiriki mashindano yajao bila kulipia ada.

Akizungumzia kuhusu maandalizi, Mkurugenzi wa Mbio, Robert Kaliyahe alisema maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa ikiwa ni pamoja na upimaji wa njia zitakazotumika kwa wakimbiaji wa mbio za kilometa 21 na zile za kilometa tano.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha katika mbio hizi,tayari tumewasiliana na wenzetu wa jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kwa ajili ya kuhakikisha usalama kwa wakimbiaji wakati wa kuanza mbio pale uwanja wa Jamhuri na baada ya mbio kuhitimishwa.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Morogoro ,Pascal Kihanga amesema mkoa wa Morogoro unakwenda kuandika historia nyingine kwa kuuingiza mkoa huo katika medani ya mchezo wa riadha kwa kuanzisha mashindano ya Morogoro Marathoni.

“Mrogoro inavivutio vingi ambavyo vimekuwa havitangazwi lakini kwa kupitia mashindano haya tutapata fursa mpya ya kutangaza vivutio vyetu ambavyo vitaendelea kuutangaza vyema mkoa wetu wa Morogoro.”alisema Kihanga .

Mbio za Morogoro Marathon 2018 zinafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Morogoro huku watu zaidi ya 3000 wakitazamiwa kuanza kukimbia kuanzia majira ya saa 12:30 na kwamba zoezi la usajili kwa wakimbiaji linaendelea katika vituo mbalimbali nchini na litafungwa saa 12:00 siku ya tukio.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: