Meneja wa huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kumtafuta mshindi wa tatu wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. ambapo mkazi wa Arusha George Issaya (29) aliibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kutoka Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Adam Kefa, na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini ,Majid Bakari.
 Meneja wa huduma za Masoko wa TBL,David Tarimo (wapili kushoto) akipofya kitufe cha Komputa wakati wa kumtafuta mshindi wa tatu na wa mwisho wa promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa. ambapo mkazi wa Arusha George Issaya (29) aliibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Droo hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Kutoka Kushoto ni Meneja Matukio wa TBL, Adam Kefa, Meneja wa huduma za Jamii wa Aim group, Aidan Mattaka na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini ,Majid Bakari.
Meneja wa huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo (kushoto) akiongea na George Issaya (29) mkazi wa Arusha mara baada ya kuibuka mshindi wa gari aina ya Renauld Kwid. Wakati Droo ya tatu ya promosheni ya TBL Kumenoga Tukutane baa iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa huduma za Jamii wa Aim group, Aidan Mattaka na msimamizi wa michezo ya Kubahatisha nchini, Majid Bakari.
---
Droo kubwa ya mwisho ya promosheni ya ‘TBL Kumenoga, Tukutane Baa’ imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha, George Isaya (29) amejishindia gari mpya aina ya Renault KWID.

Isaya akiongea baada ya kupigiwa simu na Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, kumfahamisha kuwa ameibuka mshindi, alisema anayo furaha kufanikiwa kuwa miongoni mwa washindi kupitia promosheni hiyo kwa kujishindia gari mpya. “Sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii, Habari hizi naziona kama ndoto kwangu, nashukuru TBL kwa kunifungulia mwaka vizuri na kutimiza ndoto yangu ya kumiliki gari “alisema kwa furaha.

Meneja wa Huduma za Masoko wa TBL, David Tarimo, kwa niaba ya kampuni ya TBL, alimpongeza mshindi huyo na kutumia fursa hiyo kuwashukuru wateja wote wa kampuni ambao walishiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo zawadi za magari 3 mapya ambayo yalitolewa na kampuni hiyo.

“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka kumpata mshindi wa tatu wa zawadi kubwa ya mwezi ambayo ni gari mpya. Tunawashukuru wateja wetu kutoka nchini pote walioshiriki kwenye promosheni hii ya miezi mitatu ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi uliopita”. alisema Tarimo.

Aliongeza kuwa, promosheni hii ambayo ilikuwa inafanyika kwenye mabaa katika siku za mwisho wa juma za Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, kupitia bia za chapa za Safari Lager, Kilimanjaro Lager, Castle Lite na Balimi Extra Lager imepata mafanikio makubwa kutokana na wateja wengi kujitokeza kushiriki na baadhi yao kufanikiwa kujishindia zawadi mbalimbali na hivyo TBL kufanikisha lengo lake ambalo lilikuwa ni kuwashukuru wateja kwa kuiunga mkono kampuni kupitia kununua bidhaa zake.

Kwa upande wake, Meneja wa Ukuzaji wa Masoko wa TBL, Edith Bebwa, aliwashukuru wateja wote wa TBL kwa kuendelea kuunga mkono kampuni na kuahidi kuwa promosheni mbalimbali za kunufaisha wateja wa kampuni hiyo zinatendelea kubuniwa katika siku za usoni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: