Na Mwandishi wetu Mihambwe

Afisa Tarafa Mihambwe Gavana Emmanuel Shilatu ameagiza Madarasa mawili mapya yaliyojengwa Shule ya Sekondari ya Mkoreha kumaliziwa vyema na kufunguliwa Mara moja ili Wanafunzi waanze kusomea Mara moja.

Agizo hilo amelitoa Leo Ijumaa Januari 18, 2019 alipotembelea na kukagua ulipofikia ujenzi wa Madarasa hayo akiwa amembatana na Mtendaji Kata Mkoreha pamoja na Mwalimu Mkuu Sekondari ya Mkoreha ambao pia ni Wajumbe kamati ya ujenzi Madarasa hayo.

*"Madarasa yanapendeza kiukweli. Naagiza yakamilishwe vyema kabisa na Mara moja yaanze kutumika kuanzia wiki ijayo. Nisisikie hadithi nyingine, nataka kuona Wanafunzi wanaanza kusomea Mara moja."* Aliagiza Gavana Shilatu.
Wakati huo huo Gavana Shilatu ameongea na kuwapongeza Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mkoreha ambao wamekwisha ripoti na kuanza kusoma na kuwasihi kuzingatia zaidi elimu na kupeleka salaam kwa waliochelewa kuripoti kufika shuleni haraka.

*"Nawapongeza nyote kwa kuripoti shuleni, msome kwa bidii. Pia fikisheni salaam kwa wenzenu ambao bado wapo nyumbani waje shuleni haraka iwezekanavyo."* alisema Gavana Shilatu wakati akiongea na Wanafunzi hao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: