Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola ametengua uteuzi wa Makamandaa wa polisi watatu wa mikoa ya Temeke,Ilala, na Arusha kwa makosa mbalimbali ikiwemo kujihusisha na vitendo vya Rushwa kulinda Askari wanaohusishwa katika kusindikiza utoroshwaji wa Bidhaa, na madawa ya kulevya.

Lugola ametaja Makamanda hao kuwa ni Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula na Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'azi

Waziri Lugola ametangaza uamuzi wake huo leo Jumatano Januari 16, 2019, katika mkutano na waandishi wa habari akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya kushauriana na vyombo anavyoviongoza.

Lugola pia amemtaka Kamanda Wa kikosi cha Usalama barabarani nchini kujitathmini kama anatosha katika nafasi hiyo. "Mimi ndio waziri wa mambo ya ndani ya nchi nasimamia vyombo vyote hivyo, nikitengua uteuzi inabaki kazi ya IGP kuteua mtu mwingine kujaza nafasi" amesema waziri Kangi Lugola.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: